Linah Sanga.
Wasanii wakubwa Bongo, watafanya shoo kali itakayoambatana na ujumbe
mahsusi kuhusu gonjwa hatari la Ukimwi, wakati wa kilele cha Siku ya
Ukimwi Duniani, Desemba Mosi 2013.
Linah, Barnaba, Amin, Linex, Recho, Snura, Ally Nipishe, Mataluma, Kundi la Makomando na wengine wengi, wataangusha shoo kali siku hiyo katika Viwanja vya Biafra, Kinondoni, Dar es Salaam.
Linah, Barnaba, Amin, Linex, Recho, Snura, Ally Nipishe, Mataluma, Kundi la Makomando na wengine wengi, wataangusha shoo kali siku hiyo katika Viwanja vya Biafra, Kinondoni, Dar es Salaam.
Rachel Haule ‘Recho’
Mratibu wa tamasha hilo, Paul Makonda, amesema kuwa shoo hiyo
imeandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) kwa lengo
la kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu hatari ambayo imeendelea kutanda
dhidi ya janga hilo.
“Moja wa majukumu ya UVCCM ni kusimamia ustawi wa vijana, tunajua
kwamba Ukimwi ni tishio kwa kada zote lakini vijana ni wahusika wakuu,
kwa hiyo ni lazima tukumbushane katika kuhakikisha tunautokomeza kabisa
ugonjwa huu,” alisema Makonda na kuongeza:
“Tuna orodha ya wasanii wazuri sana ambao wanapendwa na jamii, hawa
wamekubali kushirikiana na sisi, kwa hiyo watafanya shoo nzuri, bila
kusahau ujumbe kutoka kwao ambao wamewaandalia mashabiki wao kwa ajili
ya siku hiyo.”
Makonda aliongeza kwamba vilevile kutakuwa na watu mbalimbali
mashuhuri ambao watatoa ujumbe kwenye siku hiyo, akasisitiza kuwa ni
vizuri kila mwananchi akajitokeza ili aburudike na apate ujumbe mahsusi
wa kumuwezesha kujikinga na maambukizi ya Ukimwi.
“Tunasisitiza shoo hiyo haina kiingilio, yaani ni bure kabisa, watu
waje kuanzia saa 6:00 mchana maana shoo kamili itaanza saa 7:00 mchaa
mpaka saa 12:00 jioni. Ulinzi ni wa uhakika,” alisema Makonda.
No comments:
Post a Comment