Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8
Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela.
Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais
Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca
Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia
kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada
ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa
kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza
mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu
waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu,
jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais
Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina
yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo
uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja
baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela
ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa
. Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake
hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na
wananchi wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".
Mandela
amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye
aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa
rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.
CHANZO: BBCSWAHILI
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.
CHANZO: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment