Mwenyekiti
wa Bodi wa benki ya Covenant Balozi.Salome Sijaona(katikati)akibonyeza
kitufe cha kopyuta kuashiaria uzinduzi rasmi wa huduma ya” benki mtaani
kwako” ambayo inawawezesha wananchi na wateja wa benki hiyo kutumia simu
zao za kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa fedha
katika akaunti zao.Anaeshuhudia kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa
benki hiyo Bi.Sabetha Mwambenja pamoja na wajumbe wa bodi wa benki hiyo.
Mwenyekiti
wa Bodi wa benki ya Covenant Balozi.Salome Sijaona(kulia)akizungumza na
waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma
ya” Benki Mtaani Kwako” ambayo inawawezesha wananchi na wateja wa benki
hiyo kutumia simu zao za kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo
kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao.kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa benki hiyo Bi.Sabetha Mwambenja.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya Covenant Bi.Sabetha Mwambenja(katikati)akisisitiza
jambo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya” Benki Mtaani Kwako” ambayo
inawawezesha wananchi na wateja wa benki hiyo kutumia simu zao za
kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa fedha katika
akaunti zao,pamoja nae katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Balozi.Salome Sijaona(watatu kutoka kushoto) pamoja na wajumbe wa bodi wa benki hiyo.
========= ======== ========
BENKI YA COVENANT YAZINDUA HUDUMA YA BENKI MTAANI KWAKO
Dar es Salaam 9, Januari 2014. Katika
kuhakikisha inaendelea kupanua wigo na kusogeza huduma zake za kibenki
karibu na wateja wake benki ya Covernant imezindua huduma za kibenki
kwa njia ya simu inayojulikana kama”Benki Mtaani kwako” huduma hii
ambayo itawawezesha wateja wa benki hiyo kuweka na kutoa fedha katika
akaunti zao kupitia simu za Mkononi.
Akizungumza wakati
wa kuzindua huduma hiyo Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Balozi.Salome
Sijaona,amesema kuwa benki yake inawalenga watu wa kawaida kabisa ambao
wengi wao wanaishi maeneo ya nje ya mji wengi wao wakiwa wajasiriamali
na wafanyabiashara wadogo hivyo kuanzisha huduma hii ni faraja kubwa kwa
wateja wetu ambao hawatapata tabu tena ya kutoka sehemu waliko kuja
katika tawi la benki hiyo kupata huduma.
“Uzinduzi
huu umekuja wakati muafaka ikiwa ni sehemu muhimu ya kuendelea
kuboresha na kusogeza huduma zetu kwa wateja wetu, tuna wateja maeneo
mengi ya mjini na vijijini, tumeona ni jambo jema kuwaanzishia huduma
hii ambayo haita walazimu wao kuja katika tawi letu kupata huduma,
aliongeza Balozi Sijaona.
“Tunawajali
na kuwathamini wateja wetu na sasa tumewaletea huduma hii ya kuweka na
kutoa pesa kwenye akaunti zao kupitia simu za kiganjani wakiwa mahala
popote pale, wote tunatambua kuwa dunia ya sasa teknolojia ndio kila
kitu, mtu anapoweza kupata kila kitu kupitia simu yake ya mkononi ni
jambo jema kwetu, natoa wito kwa wateja wetu kutumia huduma hii ambayo
naamini ni suluhisho kwao watakapo kuwa na uhitaji wa kuweka au kutoa
fedha katika benki yetu.”
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bi. Sabetha Mwambenja
amesema amefurahi kwa benki yake kuendelea kuboresha huduma kwa wateja
wake na kuhakikisha wanafikia malengo ya huduma bora kwa wateja wake,Pia
alizitaja sifa muhimu za huduma hiyo kuwa ni kulipia Ankara
mbalimbali,kuhamisha fedha kwenda akaunti yoyote uliyokuwa nayo na
covenant benki,kuhamisha fedha kupitia mtandao wowote wa simu za
viganjani nchini,kutuma na kuchukua fedha ATM bila kadi ya benki hata
kama aliyekutumia hana akaunti na Covenant benki,kupata miamala
uliyofanyika kwenye akaunti yako na kusajili huduma hii mwenyewe kupitia
simu yako na usajili unakamilika papo hapo.
“Tunamipango
mingi ya kuendelea kupanua na kuboresha huduma zetu, hadi kufikia sasa
tunashukuru namna ambavyo wateja wetu wameendelea kutuunga mkono siku
hadi siku, tunawaahidi kuendelea kuwaunga mkono na kuhakikisha
tunatimiza ndoto zao za kuwa na maisha bora.”
Tunaendelea
kuwahamasisha Watanzania kuendelea kujiunga na huduma zetu ambazo
zinafaida nyingi kwani wateja wanaweza kutumia akaunti zao wakati
wowote,kuondoa adha ya kusafiri/kutembealea tawi la benki,kuhamisha
fedha kwa uwapendao kwa urahisi zaidi,wanaweza kuwalipa washiriki wa
biashara na wagavi bila wasiwasi,Pia hadi sasa tunazo akaunti za aina
mbalimbali ambazo ni akaunti za akiba inayojumuisha akaunti ya Ahadi,
Jerusalem, Tausi Women Entrepreneurs Account, Winner Junior account,
Vikundi, Akaunti ya Akiba ya Bajaj, Akaunti ya Muda Maalum na nyinginezo
na akaunti za biashara ni pamoja na akaunti binafsi na nyinginezo.
Ili kujiunga na huduma hiyo Mteja wa benki hiyo atatakiwa kupiga namba *150*27#
No comments:
Post a Comment