Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akiwa katika kikao na Ujumbe kutoka nchi ya Algeria wakiongozwa na Waziri wa
Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Youfsi (wa kwanza kulia)
walipomtembelea jana Ofisini kwake. Wa kwanza Kushoto ni Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo. Wengine katika picha ni Watendaji wa
Mashirika ya nishati na gasi ya Tanzania.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (katikati) katika
picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi na
ujumbe wake ( wa pili kushoto mstari wa
mbele), Wa pili kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Mhe.profesa Sospeter
Muhongo .
Na
Asteria Muhozya
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amesema Tanzania
itakuza uhusiano na ushirikiano na nchi ya Algeria kutokana na nchi hiyo kuwa
mfano mzuri kwenye uwekezaji wa rasilimali asilia.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana wakati Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe.
Youcef Yousfi alipomtembelea ofisini
kwake jijini Dar es Salaam.
Aliongeza
kuwa, Algeria ni moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa katika maendeleo ya sekta
ya nishati za gesi na umeme kutokana na kwamba sekta hiyo inachangia takribani
asilimia 60 ya uchumi wa nchi hiyo hali ambayo inatoa fursa kwa Tanzania
kujifunza na kuendeleza sekta hiyo kutoka kwao.
“Ni fursa nzuri kwetu kujua namna wenzetu
walivyoweza kufanikiwa na kuendelea kwa kutumia rasilimali hizo. Hali ambayo
imefanya nchi hii kuwa mwalimu wa Mataifa mengine yanayochipukia katika
kuwekeza katika rasilimali hizo”. Alisema.
Aidha
Waziri Mkuu aliongoza kuwa, Algeria ni nchi ya mfano kwa Tanzania ikizingatiwa
kuwa, imezisaidia nchi kadhaa za Falme za kiarabu zilizofanikiwa katika sekta hiyo ikiwemo pia nchi ya Qatar.
Akiongelea
kuhusu Serikali kumiliki uchumi kupitia sekta hizo kama ilivyo kwa Algeria,
Waziri Mkuu alisema Serikali inataka kuona nchi hii inafanikiwa katika hilo.
“Serikali
ya Algeria inasimamia asilimia 51 ya hisa katika sekta hizo kupitia kampuni za
umma, na sisi tuna makampuni kama Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (
TPDC), na Shirika la Madini Tanzania
(STAMICO) hivyo tunataka kujifunza kwa wenzetu kuona namna gani vyombo vyetu
vya umma vinavyoweza kufanya kazi kwa kuangalia mifano ya wenzetu na kukidhi
matarajio ya wananchi.” Alisema.
Kuhusu
kuendeleza rasilimali watu katika sekta hiyo, Waziri Mkuu kwanza ameishukuru
Serikali ya Algeria kwa kuendelea kutoa msaada wa ufadhili kwa wanafunzi kusoma
nchini humo, lakini zaidi hasa katika masomo ambayo ni maalumu katika sekta
hiyo.
Aliongeza
kuwa, ni funzo kwa Tanzania kuona namna gani Serikali itavitumia vyuo vilivyoko
nchini kuzalisha wataalamu wa sekta za gesi,mafuta,umeme na madini.
Vilevile
alisema kuwa anaamini wizara ya Nishati na Madini imejipanga vizuri kutekeleza
mipango na hivyo ameitaka Wizara kuhakikisha wananchi wanapata matokeo ya
haraka katika muda mfupi.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati na Migodi Algeria Mhe. Youcef Yousfi ameishauri
Serikali kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwa kuwa yanatarajia kuleta tija
kwa Tanzania huku watanzania wenyewe wakiwa na utaalamu mkubwa katika sekta
hiyo. “Tunataka
kuisaidia Tanzania kujua namna bora ya kusambaza umeme na gesi, ndio maana tuko
hapa alisema”, Waziri Yousfi.
No comments:
Post a Comment