Mtangazaji
wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr
Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke,
ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji
wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr
Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke,
ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji
wa Kipindi cha Power Breakfast, Paul James (PJ), akikabidhi msaada wa
pedi kwa mmoja wa wakina mama walio katika wodi ya wazazi wa hospitali
ya Temeke.
Msanii
wa mashairi na kughani, Mrisho Mpoto akikabidhi msaada wa pedi za
watoto kwa Mama Leah Othman katika hospitali ya Temeke ikiwa ni katika
kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji wa Jahazi, Ephraim Kibonde akimfariji mmoja wa akina mama katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Temeke.
Mtangazaji
wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akimhoji mmoja wa vijana ambao
wameacha kutumia madawa kwa msaada wa kituo cha Keko Youth. Clouds FM
ilitembelea kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 na kutoa
msaada wa mashine ya kupaka rangi kwa vijana hao
Baadhi
ya wafanyakazi wa Clouds FM wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake
waliokuwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Temeke, baada ya
kukabidhi misaada yao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds
FM.
Mtangazaji
wa kipindi cha Club 10, Perfect Chrispin akikabidhi michango ya papo kwa papo
iliyotolewa na wafanyakazi wa Clouds FM kwa kituo cha mwanzilishi wa kituo cha
Keko Youth, Yohana Victor Haule. Mbele yao ni mashine ya kupaka rangi
iliyotolewa na Clouds FM kama msaada kwa kituo hicho.
Mwanzilishi
wa kituo cha Keko Youth, Yohana Haule akimkabidhi zawadi ya kuku Meneja wa Vipindi wa Clouds,
Seba Maganga, ikiwa ni kama shukrani kwa kutembelea kituo chao.
========= ======= ========
Miaka 14 ya Clouds FM yaadhimishwa kwa shwangwe kubwa
- Shughuli za kijamii na burudani zatawala
Kituo cha Redio namba moja hapa nchini, Clouds FM kimefikia kilele cha mwezi wa maadhimisho ya miaka 14 toka kimeanzishwa. Maadhimisho
hayo ambayo yamefanyika kwa mwezi mzima sasa, yalianza na watangazaji
wa vipindi tofauti kwenda mikoa mbalimbali ili kuweza kusherekea miaka
hii 14 pamoja na wasikilizaji wao sehemu walipo.
Ikiwa
ndio siku ya kilele cha maadhimisho hayo, Clouds FM imetembelea
hospitali ya Temeke na kituo cha kuhudumia vijana wanaotumia madawa ya
kulevya cha Keko Youth, ambapo misaada mbalimbali imetolewa. Wakiwa
katika hospital ya Temeke, Clouds FM imetoa vifaa mbalimbali vya
hospitali katika wodi ya wanawake na watoto, huku Keko Youth wakipewa
vitendea kazi ambavyo vitawezesha vijana kujiajiri baada ya kumaliza
matibabu.
Akizungumzia
maadhimisho hayo ya Clouds FM, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media
Group, Joseph Kusaga alisema sherehe hizi kwa mwaka huu ni za kipekee
kwa Clouds FM hasa kwa kuwa wameweza kufanikisha mambo mengi makubwa
toka walipoanza. ‘Maadhimisho
haya ya miaka 14 kwa mwaka huu yana lengo moja kubwa, kuwashukuru
wasikilizaji wetu kwa kutufikisha hapa tulipo, na ndio maana tumeanza
kwa kuwapa misaada wanaohitaji, halafu tunamalizia kwa burudani’’
alisema Kusaga.
Akielezea
zaidi mafanikio ya Clouds FM kwa kipindi cha miaka 14, Kusaga alisema
redio imefanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi, imeongeza ubunifu lakini
pia kumekuwa na uboreshaji wa hali ya juu wa mitambo ya kutangazia
pamoja na maudhui.
‘Kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo tumefanikiwa kushinda tuzo ya Super
Brand, na kwa mwaka huu pekee radio imefanikiwa kuanza kusikika mikoa ya
Njombe, Songea, Njombe, Sumbawanga, Katavi na Geita, kupitia mitandao
kwa wasikilizaji wetu nje ya nchi lakini pia tumefanikiwa kufanya
tamasha la Fiesta kwa mafanikio zaidi’ alisema Kusaga.
Kusaga
pia aligusia mchango wa Clouds FM katika kuhamasisha maendeleo na
uzalendo hapa nchini akitoa mfano wa semina za Fursa ambazo zilifanikiwa
kwenda nchi nzima zikizungumza na vijana kuamka na kuchangamkia fursa
katika sehemu wanazoishi. ‘Semina
za Fursa zimekuwa mfano mkubwa namna Clouds FM ilivoweza kutumia nguvu
yake kama radio inayosikilizwa zaidi katika kuchagiza maendeleo, na kwa
hakika mafanikio ya semina yamekuwa ni makubwa sana’ alisisitiza Kusaga.
Kusaga
pia alitoa shukrani za pekee kwa watanzania kwa kuinga mkono Clouds FM
sio kwa kusikiliza tu bali hata katika kuhudhuria matamasha na shughuli
nyingize za Clouds. Kilele cha
maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM kitamalizika kwa burudani kubwa
ambayo itafanyika katika viwanja vya Mwembeyanga ambayo itajumuisha
wasanii na watu wengine maarufu.
‘Kumekuwa
na mafanikio makubwa katika redio yetu kwa kipindi cha miaka 14, na
naomba niseme, bila ninyi wasikilizaji wetu tusingeweza kufika hapa’
alimaliza Kusaga
No comments:
Post a Comment