ALIPOPANDA basi kutoka Tanga kuelekea Dar es Salaam mwezi fulani
mwaka 1984, hakujua kama ilikuwa ni siku yake ya mwisho kuwa mzima,
mwenye mwili mkakamavu uliokamilika viungo vyote.
Akiwaacha
nyuma mkewe, Veneranda Makamba na watoto wake wawili, Bashangi
(aliyekuwa na umri wa miaka 12) na James (10), Francis Benard aliyekuwa
na umri wa miaka 46 wakati huo, uzima wake ulikomea maeneo ya Mto Wami,
ambako alipata ajali iliyomlaza kitandani akiwa mahututi katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa miaka sita.
Hadi
wakati akipata ajali hiyo, Francis alikuwa mjasiriamali, hivyo tukio
hilo liliharibu kabisa mfumo mzima wa maisha yake kiuchumi.
Na bahati mbaya nyingine, akiwa hospitalini hapo, mkewe Veneranda alifariki dunia na hivyo kusababisha watoto wake kulelewa na watu asiowafahamu hadi leo akiwa na umri wa miaka 75.
Na bahati mbaya nyingine, akiwa hospitalini hapo, mkewe Veneranda alifariki dunia na hivyo kusababisha watoto wake kulelewa na watu asiowafahamu hadi leo akiwa na umri wa miaka 75.
Mzee Francis amepooza sehemu kubwa ya mwili wake, hali inayomfanya
awe mtu wa kulala tu na akibadilisha sana ‘style’ basi ni kukaa. Hawezi
kusimama, hawezi kutembea na hana hata ndugu. Kwa miaka 29 sasa anaishi
na watu asiowafahamu.
Baada
ya kukaa kwa miaka mingi hospitalini hapo akiwa katika hali hiyo,
ambayo mwenyewe aliielezea kama kupata nafuu, alihamishwa na kupelekwa
katika kituo cha kuhudumia watu wasiojiweza kinachojulikana kama Kwa
Mama Theresa, kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.
“Nikiwa nimelazwa pale Muhimbili, nilijifunza kufuma maua na vitambaa
kiasi kwamba baadhi ya wagonjwa wenzangu wakanitambua. Wakawa wanakuja
kwangu wananunua. Hadi napelekwa Mburahati nilishakuwa maarufu na nikawa
na wateja wengi.
“Sasa nilipohamishiwa kule, wateja wangu wakawa wanaendelea
kunifuata, kitendo kile kikawaudhi baadhi ya wenzangu wa pale, wakaanza
kuninunia, wakawa wananinyima baadhi ya vitu,” anasema mzee Francis.
Baada
ya kuona hali inazidi kuwa mbaya kwa upande wake, alisema aliamua
kukodi teksi kwa fedha kidogo alizozihifadhi na kuelekea Muhimbili
ambako alipewa tena kitanda hadi sasa.
Anawashukuru sana wauguzi na
uongozi wa hospitali hiyo ya taifa, kwani wanamtunza vizuri, licha ya
taabu kubwa ya kimwili anayoipata.
Mzee Francis yupo wodi namba 14 katika Jengo la Kibasila na kidogo
kidogo bado anaendelea kujikimu kwa namna hiyo ya kufuma na kutengeneza
maua, ambayo pia yamemfanya kupata marafiki.
MSAADA
Kutokana na uwezo wake wa kujua kufuma vitambaa na kutengeneza mapambo mengine ya urembo, mzee huyo anaomba kuwezeshwa zaidi ili aweze kujiongezea kipato.
Kutokana na uwezo wake wa kujua kufuma vitambaa na kutengeneza mapambo mengine ya urembo, mzee huyo anaomba kuwezeshwa zaidi ili aweze kujiongezea kipato.
Na kwa vile ajali hiyo ilimfanya ashindwe kusimama wala kutembea,
anamuomba Mtanzania yeyote kumsaidia baiskeli ya walemavu ili aweze
kutembelea ambayo alisema amesikia kuwa zinauzwa shilingi laki nane za
Kitanzania.
Kwa aliyeguswa na tatizo la mzee huyu anaweza kwenda Hospitali ya
Muhimbili wodi 14 Kibasila au kuwasiliana naye moja kwa moja kupitia
simu yake namba 0653313804.
CREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment