NYAKATI za mwanzo wa uhusiano, huba na kila aina ya manjonjo kwenye
mapenzi hutawala. Huwa na vitu vingi sana vya kuvutia, visivyochosha. Ni
rahisi kuwasikia wenzi wakilaumiana kwa kutokuamshana asubuhi!
Yeah!
Ni mambo ya mwanzo hayo. Ni ukweli ulio wazi kuwa, katika siku za
mwanzo za wapenzi kukutana na kufahamiana, kila mmoja huwa makini
kuhakikisha hamuudhi mwenzake.
Kila kitu hufanyika kwa umakini huku akizingatia kuwa kuna mtu
mwingine katika maisha yake. Hataki kumkwaza mtu ambaye ndiye furaha
yake. Kwa maneno mengine, kuchukia kwake, kutamfanya hata yeye akose
furaha pia.
Hiyo ndiyo sababu kubwa hasa zinazowafanya wengi kuwa makini na
uhusiano kuwa wenye nguvu. Ilivyo ni kwamba, baadaye uhusiano
ukishachangamka na kufikia angalau mwaka mmoja au zaidi, kuna mambo
yatabadilika.
Tayari hawa ni marafiki wakubwa, ambao kwa namna moja au nyingine
wanafahamiana kwa karibu zaidi na pengine wameshaanza kuzoeana sasa.
Marafiki, huo ndiyo ukweli wenyewe ulivyo.
Mfano niliotoa hapo juu, unafanana kabisa na hata kwa upande wa
wanandoa. Siku za mwanzo wa ndoa huwa kuna vitu vinakuwa na mguso na
mvuto wa aina yake lakini siku zinavyozidi kwenda, ndivyo baadhi ya
mambo huanza kubadilika taratibu.
Ni mfumo. Hakuna cha ajabu. Hata hivyo, yapo mambo ambayo hupaswa
kuzingatiwa ili penzi liendelee kudumu. Kweli kuna kupishana baadhi ya
maeneo lakini sasa yasisababishe maisha yashindwe kuendelea mbele.
Hapa kwenye Love & Life tunazingatia kwamba, maisha ni mtindo
ambao huchaguliwa na mhusika mwenyewe. Kwa mfano, ukiamua kumnunia mkeo
au mumeo kwa sababu amefanya jambo fulani ni sawa na kulazimisha
‘stress’ ambazo si za lazima.
Kwa nini usishughulikie tatizo likaisha mara moja? Marafiki zangu,
hasa wale ambao ndiyo kwanza mmeingia kwenye ndoa hivi karibuni
(namaanisha kuanzia siku moja – miaka mitatu), lazima mjitahidi
kutofautisha maisha ya ndoa na yale ya urafiki na uchumba.
KWA NINI HASA?
Sababu za msingi zaidi nimezieleza hapo juu. Lakini jambo kubwa la kuongezea hapa ni kwamba, mnapokuwa kwenye ndoa, mnapaswa kufahamu kuwa mmejiunganisha kwa ajili ya maisha yenu moja kwa moja.
Sababu za msingi zaidi nimezieleza hapo juu. Lakini jambo kubwa la kuongezea hapa ni kwamba, mnapokuwa kwenye ndoa, mnapaswa kufahamu kuwa mmejiunganisha kwa ajili ya maisha yenu moja kwa moja.
Wakati fulani mume anaweza kuwa bize akihangaika na kufikiria
kufanya kazi pengine zaidi ya tatu kwa wakati mmoja ili familia yake
ijiendeshe sawasawa. Si rahisi muda wote kukawa na mahaba yale
yaliyokuwa zamani.
Sawa, ni vyema kutenga muda wa kukaa na mwenzako na kufurahia maisha.
Hapo mnaweza kuamua kutoka au pengine hata kama ni mazingira yaleyale
lakini kwa staili tofauti na siku nyingine.
Kikubwa ni kuwekeza upendo wako wa dhati moyoni mwako na ujihakikishie kuwa uliridhika naye kabla ya kuingia kwenye muunganiko huo. Upendo ndiyo umebeba kila kitu.
Kikubwa ni kuwekeza upendo wako wa dhati moyoni mwako na ujihakikishie kuwa uliridhika naye kabla ya kuingia kwenye muunganiko huo. Upendo ndiyo umebeba kila kitu.
MAHITAJI
Kuna baadhi ya wanandoa (hasa wanawake) wamekuwa na tabia ya kuwalalamikia waume zao kuwa hawawapatii mahitaji yote ya muhimu kama zamani. Utakuta mwanamke anataka nguo mpya kwa mfano, anataka kupelekwa ufukweni au kwenye bendi.

Hayo ni mambo ambayo mumewe alikuwa akiyafanya wakati wa uchumba wao
lakini sasa amebadilika. Jambo la kujiuliza, ni je, kuna tofauti ya
tabia kati ya wakati huo na sasa?
Je, muda ambao umekuwa ukienda naye kwenye bendi ndiyo anaoutumia huko nje sasa hivi? Hapa naomba nifafanue zaidi. Lakini nje inategemea na mahali anapokuwa. Mathalani yupo kwenye mihangaiko ya kutafuta fedha, si kosa.

Kumbuka sasa mpo kwenye ndoa, starehe si muhimu sana kama kujali familia na kutatua matatizo kwa haraka.
Siyo sawa kulalamika kwa kutotimiza baadhi ya mambo. Rafiki yangu,
hataweza kufanya kila kitu, lakini pia kushindwa huko kusiondoe mapenzi
ambayo yamejengeka moyoni mwako. Ridhika. Mpo kwenye mpambano wa maisha.
Wiki ijayo nitakuwa hapa kwa ajili ya kuhitimisha mada hii, USIKOSE!
Wiki ijayo nitakuwa hapa kwa ajili ya kuhitimisha mada hii, USIKOSE!
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment