Safari hii iko kimataifa zaidi ambapo wiki iliyopita ilitua huko
Hong Kong, China na kunasa ufuska wa wanawake wa Kibongo wanaokwenda
nchini humo kwa kigezo cha biashara kumbe wanakwenda kuuza miili.
Baadhi ya mastaa wa Bongo wakikata mauno nchini China.
OFM ilipata taarifa kutoka kwa chanzo chake ndipo ikatuma kachero
wake nchini humo na kujionea vitu vinavyochafua taswira ya Tanzania nje
ya nchi hasa China kama wanadada hao wanavyofanya uchafu tena wengi wao
Bongo ni mastaa.
“Kiukweli ni aibu! Wanawake wa Kibongo wanachezewa makalio hovyo,
wanafanya vitendo vya ngono hadharani kwa ujira wa dolari za Kimarekani
mia tu.
“Kuna msanii wa Bongo muvi aliyefulia ambaye ni mke wa mtu (mcheza
soka wa kimataifa) hadi sasa yupo China, nimemuona kwa macho yangu klabu
akichezewa makalio kwa dola mia moja,” alisema OFM wetu.
Uchunguzi wa OFM ulibaini kwamba kuna makundi ya wanawake wa Kibongo
wanaokwenda China wakijifanya wafanyabiashara lakini wengi wao
hubebeshwa madawa ya kulevya ‘punda’ kisha huwa hawataki kurudi Bongo
huku kukiwa na wengine wanaokwenda maalum kwa kujiuza.
Ijumaa
Wikienda liliwasiliana na staa wa Kibongo aishie nchini humo, Rehema
Fabian ambaye ni Mshiriki wa Miss Kiswahili 2009 ambaye alikiri kuwepo
kwa mastaa na wabongo wengi wanaojiuza nchini humo.
Alipotafutwa Balozi wa Tanzania nchini humo, Abraham Shimo ili kupata
undani wa ishu hiyo, simu yake ya ofisini ilikuwa ikiita bila
kupokelewa hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.
No comments:
Post a Comment