EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, February 28, 2014

JOKATE ULOKOLE BASI!

Picha za nusu utupu ambazo amezipiga mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo zinaonekana kumtesa kufuatia baadhi ya waumini wa kanisa analosali kumsema kuwa anakwenda kinyume na maadili.
Picha hizo anazoonekana amevaa gauni refu jekundu huku likiwa na mpasuo ‘wa haja’ uliyolifanya sehemu kubwa ya paja lake kuwa wazi, zimesambaa kiasi cha kuwafanya baadhi ya mashabiki wake kumtaka ajiangalie upya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wadau wamesema kutokana na jinsi alivyokuwa ametulia kiimani, mrembo huyo alikuwa anaelekea kwenye ulokole lakini kwa hili anapotea.
“Unajua yule ni modo mwenye jina kubwa sana lakini alikuwa ametulia sana, hata nilipomuona amejiunga na kwaya ya pale kanisani kwetu St. Peter, niliona ameamua kumfuata Yesu kikwelikweli lakini kwa picha hizi, mh!” alisema Juster John anayesali kanisani hapo.

DTBi - COSTECH WATILIANA SAINI YA USHIRIKIANO NA SILION VALLEY YA MAREKANI‏

Mr Carl Davis Jr, President of the Silicon Valley Black Chamber of Commerce and Eng. George Mulamula, CEO of DTBi sign MOU copy
Bw.Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi (kulia) wakisaini MOU.
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
KAMPUNI tanzu ya Tume ya sayansi na teknolojia ya DTBi-COSTECH na Silicon Valley Black Chamber of Commerce’s Center for Entrepreneurial Development (SVCED) wametiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) ambapo pande zote mbili zitashirikiana kwa njia mbalimbali kwa ajili ya ukuaji wa wajasiriamali.
Mkataba huo, kati ya DTBi na SVCED utawezesha pande hizo mbili kukuza ujasiriamali na kujenga uwezo katika Habari, Teknolojia na Mawasiliano kwenye sekta zote za kiuchumi.
Mkataba huo wa MoU utawafanya wadau kufanya shughuli za biashara kwa kuanza na mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kupitia njia ya mtandao na kusaidia wale walio na ubunifu katika nyanja mbalimbali za biashara.
Mr Carl Davis Jr, President of the Silicon Valley Black Chamber of Commerce and Eng. George Mulamula, CEO of DTBi shake hands after signing MOU copy
Bw. Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi kupeana mikono baada ya kusaini MOU.
Mkataba huo pia utasaidia wajasiriamali kuweza kukua na kufanya biashara kwa kutumia mifumo habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ujasiriamali na kuanzisha mfumo wa kubadilishana uzoefu katika kuendeleza biashara na ukuaji wa ujasiriamali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Injinia. George Mulamula amesema mkataba MOU utatoa ushirikishiano ambao utaruhusu wajasiriamali wa Tanzania kufaidika na ujuzi, maarifa ya Silicon Valley ya ujasiriamali.
Amesema hii itasaidia nchi ya Tanzania kuruhusu uanzishwaji wa biashara kupitia njia ya mtandao na mifumo ya Habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ajira na kuchangia pato la taifa.
Mr Mulamula explains the partnership to the press copy
Eng.George Mulamula akielezea ushirikiano kwa vyombo vya habari.
Baada ya kutiliana saini ya MOU, Bw Carl Davis Jr, alikuwa na semina kwa wajasiriamali yenye jina la “The Mindset of the Silicon Valley Entrepreneur: Lessons for the Tanzania Entrepreneur/Innovator”.
Mr Davis Jr amesema anaweza kuwasaidia “wajasiriamali kuelewa jukumu la uzinduzi na ujasiriamali na jinsi Wajasiriamali hapa nchini jinsi wanavyoweza kujiinua katika kufikiri chanya kwenye maeneo ya biashara.

MWIGULU NCHEMBA AZINDUA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA KALENGA‏

Naib Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Mwigulu Nchemba akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ifunda mkoani Iringa, ambapo CCM ilizindua rasmi kampeni katika jimbo la Kalenga wakimnadi mgombea wao kwa tiketi ya chama hicho Bw. Godfrey Mgimwa na kuwaasa wanakalenga kumchagua Godfrey Mgimwa kwani ni mwakilishi wao kamili kutokana na kwamba ilani inayotekelezwa mpaka mwaka 2015 ni ya Cmaha cha Mapinduzi hivyo Mgimwa ataisimamia vyema na kukimalizia kipindi cha miezi ishirini iliyobaki kwa maendeleo ya wanakalenga. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IFUNDA)Mwigulu akimnadi Geofrey Mgimwa leo(1) 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Mwigulu Nchemaba akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga Gedfrey Mgimwa, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ifunda, Iringa Vijijini. (Picha na Bashir Nkoromo)
2 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Mwigulu Nchemaba na mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa wakifurahia jambo kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika kata ya Ifunda,kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu.

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUKONGA NYOYO MASHABIKI ZAKE, NI IJUMAA HII TENA PALE THAI VILLAGE‏


DSC_0303
Joniko Flower akiongoza safu ya Skylight Band kutoa burudani kwa mashabiki wa Bendi hiyo Ijumaa iliyopita kwenye kiwanja chao cha Nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar.... Ni kila Ijumaa zote za wiki wanakuwa hapo kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wake!!!
DSC_0229
DSC_0244
Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47 na Winfrida Richard wakiwajibika jukwaani kuwapa utamu mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0253
Hashim Donode na Winfrida Richard wakitawala jukwaa huku wakisindikizwa na Digna Mbepera pamoja na Mary Lucos.
DSC_0173
Madiva wa Skylight Band wakisaka Dough....... Kutoka kushoto ni Winfrida Richard, Mary Lucos na Digna Mbepera.
DSC_0284
Babu Athumani akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.

MKOSAJI MKUU WA HAKI ZA BINADAMU NI SERIKALI - JAJI MSTAAFU MIHAYO‏

Mjumbe wa Bodi ya Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (Tanzania Human Rights Defenders Coalition) Dkt. Hellen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha watetezi wa Haki za Binadamu nchini na Jeshi la Polisi jijini Dar leo.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdurahman Kaniki, akitoa hotuba yake ya ufunguzi kwa niaba ya IGP Ernest Mangu, kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, umuhimu wa kushirikiana kati ya Jeshi hilo na Asasi za kutetea Haki za Binadamu ili kuleta tija katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Sehemu ya makamishina na makamanda wa mikoa na maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku moja jijini Dar es Salaam.
Naibu Inspekta General wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki (kushoto), Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oparesheni, Kamishina Paul Chagonja wakifuatilia mbalimbali ilizokuwa ikitolewa na washiriki wa warsha hiyo.
Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake juu ya Ulinzi na utawala wa haki za binadamu kwa mashirika ya watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na Polisi.
Pichani juu ni Meza kuu na chini ni Baadhi ya Wakuu na Makamishina wa Jeshi la Polisi nchini wakifurahia jambo wakati wa uwasilishwaji wa mada mbalimbali kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
DSC_0362
Kamishina wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova akichangia mada katika warsha ya siku moja kuhusu Haki za Binadamu na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Kamanda wa Polisi, Arusha Liberatus Sabas akizungumza umuhimu wa kujali pia askari polisi kwa sababu na wao pia ni Binadamu wanahitaji utetezi kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea Haki za Binadamu nchini.
DSC_0390
Kamanda wa Polisi, Lindi, RPC Zeloithe Stephen akitoa nasaha kuhusu miiko na kanuni za Jeshi la Polisi jinsi zinavyotetea na kulinda Haki za Binadamu (Police General Order).
DSC_0438
Picha ya pamoja kati ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini na mgeni rasmi Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini.

Thursday, February 27, 2014

KINGWENDU AJA NA FAZA HAUSI


MSANII wa filamu nchini Athumani Lali 'Budege' baada ya kucheza filamu za watu sasa ameamua kuja na filamu zake mwenyewe na kuwawezesha wasanii wenzie kuwa na kipato kizuri baada ya kuamua kufungua kampuni yake binafsi inayokwenda kwa jina la AJM Entatainment ambayo ina husika na maswala ya filamu za kibongo

NAPE AUNGURUMA SHINYANGA AWAZOA WAWILI KUTOKA CHADEMA Thursday, February 27, 2014 Maoni: 0 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano wakati yakiingia uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa Shinyanga mjini. Wakazi wa Shinyanga mjini wakiwa na Furaha ya kuwakaribisha wanachama wapya ambao walikuwa madiwani kwa kupitia Chadema ambao tarehe 25 walijiuzuru na tarehe 26 Februari 2014 kujiunga na CCM. Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Masekelo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo na kuwaambia wananchi hao ameamua kurudi CCM kutokana na ufisadi na ukiukwaji ya maadili ya Uongozi ndani ya Chadema. Sebastian Peter maarufu kama Obama aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Ingokole akihutubia wananchi kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsaidia kufunga vifungo vya shati Ndugu Sebastian Peter aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ingokole ambaye amerudisha Kadi yake ya Chadema na kupokelewa rasmi CCM kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjni Shinyanga. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia Huu ndio Mwanzo tu,aliwaambia CCM imejengwa kwa misingi imara hivyo itaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa ushauri Mbunge wa Shinyanga Mjini Ndugu Stephen Masele juu ya VETA mkoani hapo kutoa kozi zinazoendana na mahitaji ya Soko la Viwanda vya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini tarehe 26 Februari 2014. TAARIFA YA KUPOTEA KWA BIBI HUSNA NCHINI MALAYSIA . Thursday, February 27, 2014 Maoni: 0 Tunamtafuta Bibi Husna ambaye asili ya kimalaysia, aliolewa na Mtanzania Baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa ni Bw. Said Abdullah Belwal. Kwa taarifa Husna ni Muuguzi (Nurse) ila haifahamiki hospitali gani na mji gani. Mume wake ni Mwanajeshi na ndoa yao ilifungwa kijeshi. Tafadhali atapopata tangazo hili au yeyote mwenye taarifa zake awasiliane na namba hizi Mob: +60102987357 Tel: +60342517603 Kuala Lumpur, Malaysia Email: apoloniamwangosi@yahoo.com KINGWENDU AJA NA FAZA HAUSI Thursday, February 27, 2014 Maoni: 0 MSANII wa filamu nchini Athumani Lali 'Budege' baada ya kucheza filamu za watu sasa ameamua kuja na filamu zake mwenyewe na kuwawezesha wasanii wenzie kuwa na kipato kizuri baada ya kuamua kufungua kampuni yake binafsi inayokwenda kwa jina la AJM Entatainment ambayo ina husika na maswala ya filamu za kibongo Athumani Lali 'Budege' Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Lali amesema kuwa kwa sasa yupo katika atua za mwisho kwa ajili ya kutoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la Faza Hausi ambayo imeshilikisha wasanii wakongwe ndani yake akiwemo Mohamed Nurdini 'Chekbudi' ,Esha Buheti, Rashidi Mwishehe 'Kingwendu' Muogo Mchungu . Filamu hiyo itakayo tolewa na Kampuni hiyo ya jijini Dar es salaam itakuwa moto wa kuotea mbali kwani si ya kukosa kabisa kwa mashabiki wa filamu nchini. filamu hiyo ya Faza Hausi itakuwa mtaani wakati wowote kuanzia sasa kwani takribani vitu vyote muhimu vimeshafanyika hivyo wadau wakae mkao wa kula kwani filamu hii si yakuikosa Ambapo itapatikana Tanzania nzima nikianzia Dar es salaam na mikoa yote filamu hiyo itawafikia WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAFANYA ZIARA TBL JIJINI DAR


 Wahariri wakiwa katika picha ya pamoja a viongozi wa TBL wakati wa ziara hiyo.
 Wahariri wa Vyombo vya Habari wakitembelea eneo la upikaji bia wakati wa ziara yao iliyofanyika  kwenye Kiwanda cha Bia Tanzania cha Dar es Salaam
 Mtalaam wa Upishi Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Benjamin Budigida akitoa maelezo ya jinsi bia inavyopikwa kwa kutumia njia ya kisasa ya kompyuta  wakati wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.

MWILI WA BALOZI FULGENCE KAZAURA WAAGWA LEO KATIKA KANISA LA MT. PETER JIJINI DAR

Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura likiwa ndani ya Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam tayari kwa Ibada maalum ya kumuombea Marehemu huyo iliyofanyika mchana wa leo kanisani hapo.
Viongozi wa Kanisa hilo la Mt. Peter wakiwaongoza waomboleazaji kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiwaongoza waomboleazaji mbali mbali kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Prof. Rwekaza Mkandala (mbele) Sir George Kahama,pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.

KAJALA MASANJA ANYWESHWA SUMU


Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja.
Stori: Shakoor Jongo
STAA wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amejikuta katika hali mbaya kufuatia kunyweshwa sumu na mtu ambaye hakuweza kufahamika mara moja.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili iliyopita maeneo ya Tegeta jijini Dar katika Klabu ya Seventy One ambayo alikwenda kujiachia na marafiki zake.
Chanzo cha uhakika, kilipenyeza habari kuwa, Kajala alinyweshwa sumu hiyo kupitia kwenye glasi ambayo aliwekewa juisi ambapo haikuweza kufahamika mara moja kuwa aliwekewa kabla au baada ya mhudumu kumpa huduma.
“Unajua mambo ya klabu tena, kila mtu alikuwa bize na mambo yake, hivyo hatukuweza kugundua mara moja kuwa nani alihusika, lakini tulishangaa ghafla Kajala alijisikia vibaya hivyo marafiki zake wa karibu walimkimbiza nyumbani kwao kisha hospitali,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya paparazi wetu kuzinyaka habari hizo, Jumanne iliyopita (juzi) alimtafuta Kajala ambaye alikuwa amejipumzisha nyumbani kwa njia ya simu, akaeleza kwa shindashinda jinsi tukio hilo lilivyokuwa:
“Ilikuwa Jumapili usiku, nilikuwa nimekaa na washkaji zangu pale klabu akiwemo Mubenga, sasa niliagiza juisi pale nikaanza kunywa, funda la kwanza…la pili nikaanza kujisikia vibaya.
“Nilisikia kama kichefuchefu, nikatoka nje ambapo hali ilizidi kuwa mbaya. Marafiki wakashauri nirudishwe nyumbani, nako hali ikazidi kuwa mbaya.

AUNT WA NDOA, AUNT WA BILA NDOA MULEMULE

Katika jamii pana inafahamika kuwa mwanamke akiingia kwenye ndoa huwa anatulia na kujipanga kwa ajili ya familia na maendeleo kwa jumla.
Hali ni tofauti kabisa kwa staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson Jujuman.
Aunt ana utofauti mkubwa na wanandoa wengine kwani maisha anayoishi tangu aingie kwenye ndoa na Sunday Demonte, hayana tofauti na yale aliyokuwa akiishi kabla hajaingia kwenye ndoa miaka miwili iliyopita.
Aunt amekuwa akijiachia sehemu mbalimbali za starehe bila kujali kama ni mke wa mtu na amekuwa akikumbwa na skendo lukuki.
Hali hiyo imekuwa ikiwashangaza wengi na kujiuliza kweli ni mke wa mtu?
Katika makala haya utaona matukio mbalimbali ambayo Aunt amewahi kuyafanya tangu aingie kwenye ndoa ambayo si kitu cha kawaida kwa mwanandoa.
KUKAA NUSU UTUPU JUKWAANI
Siku chache baada ya kufunga ndoa, mwaka 2012, Aunt alikwenda kwenye shoo ya Fiesta mjini Dodoma akiwa ameambatana na Wema Isaac Sepetu na kufanya kituko cha mwaka.
Akiwa kwenye shoo hiyo, Aunt alipanda jukwaani akiwa nusu utupu ambapo alipigwa picha ambazo zilizua gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ishu ilikuwa iweje mke wa mtu afanye hivyo bila aibu?
Skendo hiyo ilimfanya Aunt na Wema kutengwa na Shirikisho la Filamu (TAFF) lakini baadaye waliomba msamaha na kupewa onyo wasirudie kuvaa hivyo na endapo wangerudia wangeondolewa kabisa kwenye listi ya wasanii wa Tanzania.
KUPIGWA CHUPA
Mwaka jana ndani ya Klabu ya Bilicanas iliyopo Posta, Dar, Aunt alipasuliwa na chupa mkononi baada ya kumkosakosa usoni na aliyetekeleza unyama huo ni mwanadada aliyejulikana kwa jina la Yvonne Maximilian ambaye kabla ya Aunt kuingia kwenye ndoa walikuwa wakimgombea mwanaume aitwaye Geofrey.
Japokuwa Aunt alishaingia kwenye ndoa bado skendo hiyo ya kutembea na huyo mwanaume ilikuwa ikimsumbua Yvonne akihisi kwamba mwanadada huyo anaendelea na Geofrey, jambo ambalo Aunt alisema siyo kweli na waliachana muda mrefu kabla hata hajaingia kwenye ndoa.
SKENDO YA KUJIUZA
Hivi karibuni Aunt alikumbwa na skendo ya kujiuza baada ya kwenda jijini Arusha akiwa ameambatana na Wema na Kajala Masanja ambako walienda kwenye shoo ya kumtambulisha msanii wa Bongo Fleva, Mirrow kutoka kampuni ya Wema ya Endless Fame Films.
Ilidaiwa kwamba nyuma ya ziara hiyo kulikuwa na mabilionea waliowaita jijini humo ambao pia walifurika kwenye shoo hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Tripple A.
KUPIGANA
Mapema mwaka huu, Aunt alijikuta akizichapa na mwanamke aitwaye Sarah Mwakapala ambaye miaka kadhaa iliyopita waliwahi kugombea naye penzi  la mwanaume aliyejulikana kwa jina la Mwilu Mwilola ‘Silva’.
Chanzo cha wawili hao kuzichapa hadi kuvuana mawigi hakikueleweka lakini Aunt alishtuka baada ya kuvamiwa na mwanadada huyo wakiwa katika sherehe kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo Victoria, Dar.
Aunt anapaswa kubadilika na kuonesha sifa za mke wa mtu.

MIMBA YA LINAH YACHOROPOKA

SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Astelinah Sanga ‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye Nagar, Amani limenyetishiwa kuwa ujauzito huo umechoropoka.
Astelinah Sanga ‘Linah’.
Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na kumfanya  Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.
“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika sana kwani mdosi wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta Linah  kupitia simu yake ya kiganjani ili kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwindishi wetu kujitambulisha, staa huyo alikata simu.
Wiki iliyopita gazeti dada na hili, Risasi Mchanganyiko la Februari 19-21, mwaka huu liliandika habari za staa huyo kunasa  ujauzito  wa mdosi huyo na alipoulizwa alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi.
“Nani kakwambia kwamba nina  mimba? Hayo ni maneno ya watu, wanasambaza mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,” alisema Linah na kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka mtaani kila siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa.
CHANZO NI GPL

LULU AANIKA MCHECHETO KIZIMBANI

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa siku alipokuwa mahakamani akisomewa kesi inayomkabili ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba, alipata mchecheto sana.
Elizabeth Michael 'Lulu'.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, siku hiyo wakati kesi ikiendelea, alipata mchecheto kiaina na kujikuta ghafla akiwaza juu ya hatima yake hivyo kuangukia katika lindi la hofu.
“Daah! Nilipata mchecheto ghafla hata sijui kwa nini, nilivuta picha ya mbali sana na kujikuta nikijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,” alisema.
Msanii huyo alisomewa shitaka lake hilo Februari 17, mwaka huu kwenye Mahakama Kuu, jijini Dar, kesi hiyo iliahirishwa hadi itakapotajwa tena baada ya msanii huyo kujibu maswali ya kweli au si kweli.

Wednesday, February 26, 2014

ZINDUZI RASMI WA KAMPENI YA TAIFA YA KUSAMBAZA UELEWA WA RASIMU YA PILI YA KATIBA YA TANZANIA KWA WANANCHI WAFANYIKA LEO KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO MLIMANI CITY‏

 Jaji Mkuu Mstaafu Mh. Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi wa uzinduzi wa Rasimu ya pili ya Katiba

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, ATEMBELEA MRADI WA MAJIKO SANIFU NA KUZURU KABURI LA SOKOINE MONDULI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange juu ya kusafisha na kuyafanya maji kuwa salama, wakati alipotembelea sehemu ya karakana hiyo inayotumia umeme wa nguvu za jua (Solor Power Energe) February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Bw. Kisioki Moitiko kuhusu utengenezaji wa majiko hayo, wakati alipotembelea kwenye karakana hiyo February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya kwanza Marehemu Edward Moringe Sokoin wakati alipozuru kijijini kwa marehemu Monduli juu alipokua katika ziara ya kikazi Wilayani Monduli Mkoani Arusha February 25-2014.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekua Waziri Mkuu wa awamu ya kwanza Marehemu Edward Moringe Sokoine, wakati alipozuru kijijini kwa marehemu Monduli juu Mkoani Arusha February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka ndani ya moja ya nyumba zinazotumia majiko sanifu wakati alipotembelea katika kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha February 25-2014.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akicheza ngoma ya kimasai na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani arusha walipofika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao February 25-2014.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Dkt. Binilith S. Mahenge, akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani Arusha, ambapo ameambatana na Makamu wa Rais kwenye ziara hiyo.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani arusha walipofika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kifimbo kutoka kwa wazee wa kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha February 25-2014, mara baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kabila la kijiji hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange, February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha baada ya kuwahutubia mkutano wa hadhara February 25-2014. (Picha na OMR)

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate