- Ofisa Mtendaji akatwa mapanga
- Mbunge CHADEMA, makada 16 wapanda kizimbani
KAMPENI za uchaguzi mdogo wa madiwani zimeingia katika hatua mbaya baada ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ubagwe, Alphonce
Kimaro, kukatwa mapanga, huku Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi, akipandishwa kizimbani.
Wengine waliopandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwajeruhi wafuasi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni pamoja na Diwani wa Kata ya Buselesele,
wilayani Chato, mkoani Geita, Christian Kagoma na makada wengine 15
wanaodaiwa kuwa wa CHADEMA.
Washitakiwa hao walikamatwa juzi na kufikishwa mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Gadiel Mariki jana na kila mmoja kusomewa mashitaka sita.
Mwendesha Mashtaka wa Mahakama, Shukrani Madulu, alidai kuwa
washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo juzi katika Kata ya
Ubagwe.
Alidai kuwa washtakiwa hao wakiongozwa na Mbunge Kasulumbayi
waliwashambulia kwa mapanga wafuasi wa CCM wakati wa kampeni za udiwani
wa Kata ya Ubagwe iliyopo Halmashauri ya Ushetu.
Alidai kuwa katika vurugu hizo washtakiwa, pia walilishambulia gari la CCM la wilaya na kuliharibu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka, lakini wamenyimwa dhamana kwa
madai kuwa watu waliowajeruhi wako katika hali mbaya, kwani baadhi yao
wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kutoka Hospitali ya
Wilaya ya Kahama. Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo.
Kabla ya kufikishwa mahakamani, walioshuhudia vurugu hizo walieleza
kuwa majeruhi hao walikumbwa na mkasa huo wakati wakiwa kwenye gari la
CCM wilaya ambalo pia lilikuwa na watuhumiwa watatu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa
CHADEMA, waliokuwa wakipelekwa kituo kidogo cha Polisi Bulungwa.
Watuhumiwa hao walidaiwa kufanya fujo kwenye mkutano wa kampeni wa Chama cha TADEA ambacho pia kimeweka mgombea wa udiwani katika Kata ya Ubagwe.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kahama watu 16 akiwemo Mbunge wa Maswa
Mashariki, Kasulunabayi, walikamatwa na Polisi wakidaiwa kuhusika na vurugu hizo.
Mashariki, Kasulunabayi, walikamatwa na Polisi wakidaiwa kuhusika na vurugu hizo.
Baadhi ya majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Mji
wa Kahama akiwemo dereva wa gari la CCM Wilaya ya Kahama, Charles Peter, walisema walipofika kwenye kizuizi hicho walisimama ndipo wafuasi wa
CHADEMA waliposhuka kwenye gari la mbunge huyo na kuanza kuwapiga.
wa Kahama akiwemo dereva wa gari la CCM Wilaya ya Kahama, Charles Peter, walisema walipofika kwenye kizuizi hicho walisimama ndipo wafuasi wa
CHADEMA waliposhuka kwenye gari la mbunge huyo na kuanza kuwapiga.
Ilielezwa kuwa Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Alphonce Kimaro,
alikumbwa na sekeseke hilo kwani alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa
ndani ya gari la CCM akiwasindikiza watuhumiwa hao Polisi.
“Mtendaji huyo ni mmoja wa majeruhi waliojeruhiwa vibaya kwa kukatwa
mapanga ovyo mwilini na watu wengine watano wamejeruhiwa katika tukio
hilo na hali zao ni mbaya,” alisema Peter.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama, Richard
Mabagala, aliwataja majeruhi wengine kuwa ni pamoja na Katibu Mwenezi wa
CCM, Masuod Melimeli (34), Sebastian Masunga (34) na Ramadhani Salumu
(24).
Wengine ni Subira Nyangusu, pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ubagwe, Kimaro na dereva wa gari la CCM, Peter.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Andrew
Emmanuel, Masunga Kamaro na Peter walisafirishwa kwenda Hospitali ya Bugando
jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Emmanuel, Masunga Kamaro na Peter walisafirishwa kwenda Hospitali ya Bugando
jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment