MKUU
wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest
Mangu, amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa
upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na
watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la
Polisi.
Taarifa ya Jeshi la Polisi kwa vyombo vya habari iliyotolewa na
Msemaji wa jeshi hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Advera Senso,
ilieleza miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni
aliyekuwa Kamanda wa Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Manyara wakati aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ruvuma.
Wengine ni aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi
wa Polisi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,
aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Suzan Kaganda anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora na
aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wengine waliohamishwa ni aliyekuwa Mkuu
wa Upelelezi Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kikosi cha Tazara.
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa
Ilala na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala,
Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) Juma Bwire anakwenda kuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora.
Aidha, aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora, Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi (SSP) John Kauga anakuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Tabora,
aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Rombo, Mrakibu
Mwandamizi wa
Polisi (SSP) Ralph Meela anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mtwara
na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kikosi cha Tazara, Mrakibu wa Polisi
(SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Pwani.
Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani
waliohamishwa ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula anahamia Trafiki Kanda
Maalumu Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP)
Awadh Haji anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni na Mrakibu
wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, Mrakibu wa Polisi
(SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe,
aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe
Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP)
Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani na
aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu
wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha
wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.
No comments:
Post a Comment