EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, February 7, 2014

WEMA, AUNT, KAJALA: AIBU YAO!

Jambo limezua jambo! Mastaa ‘hot’ Bongo wanaotingisha kwenye tasnia ya sinema, Kajala Masanja, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamepata aibu baada ya kugandwa na skendo ya kwenda kujiuza jijini Arusha.
Mastaa wa filamu kutoka kushoto ni Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja.
Skendo hiyo ilikuja baada ya mastaa hao kutimba jijini humo ikiwa ni ziara ya kwenda kumtambulisha msanii wa Bongo Fleva anayesimamiwa na kampuni ya Wema ya Endless Fame Films aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow.
ETI WALIITWA NA MABILIONEA WA ARUSHA
Habari za chini kwa chini zilidai kwamba nyuma ya ziara ya mastaa hao kulikuwa na msukumo wa mataita (mabilionea wa Arusha) ambao waliwaita ili ‘wajilie vyao’.
“Kuna mtu alipewa tenda awapeleke akina Wema na kweli walifanikiwa kuwateka matajiri wa Arusha.
“Nakwambia mapedeshee wa mawe (madini) waliposikia tu watoto (akina Wema) wapo Arusha walifurika pale Club Tripple A na baadaye hotelini walikofikia pale Point Zone maeneo ya Mianzini.
 
Mastaa Wema, Aunt na Kajala wakionyesha maungo yao.
“Shughuli za kisanii, sijui eti kumtambulisha Mirrow ilikuwa ni gia tu ya kwenda kuwaburudisha mapedeshee wa A Town,” kilidai chanzo chetu ambacho huwa hakichezi mbali na mastaa hao na kuongeza:
WALIVAA KIHASARA MNO
“Wewe angalia tu walivyokuwa wamevaa kihasara, lengo lao lilikuwa ni kuwatega wanaume.”
‘Kikulacho’ huyo aliendelea kudai kwamba mastaa hao wakiwa Arusha, namba zao ziligeuka ishu baada ya kuuzwa kwa bei mbaya kwa kila tajiri aliyehitaji.
“Nakwambia hata ungetokea ukasema una namba ya mmojawapo ungelamba mshiko mrefu maana kuna shosti yao mmoja aliondoka na fedha ndefu kwa kutoa tu namba zao,” alisema na kuongeza:
“Aisee hata pale hotelini wahudumu walisumbuliwa sana kutumwa kwenda kuomba namba za simu za akina Kajala.”
WENYEWE WAFUNGUKA
Baada ya kujazwa madai hayo, gazeti hili lilizungumza na mastaa hao mmoja baada ya mwingine ambapo wote walinena juu ya skendo hiyo.
Mastaa wakipozi kitandani pamoja na Mtangazaji Zamaradi.
KAJALA

Akizungumzia ishu hiyo baada ya kupewa mkanda mzima, Kajala alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza haiingii akilini kabisa, nitoke Dar niende Arusha kujiuza kwa sababu gani? Au kwa ajili gani? Sisi ni watu ambao tunajiheshimu, mtuone hivihivi.

“Tunajua tulienda Arusha kwa sababu gani na ndicho tulichokifanya na si vinginevyo.
“Kuhusu nguo tulizovaa, mbona ndiyo mavazi yetu ya kawaida sana? Siku zote tunavaa hivyo jamani, wanaosema tulitaka wanaume hawana jipya.
“Kuhusu namba zetu kuuzwa, watu watakuwa ni wao maana sisi muda mwingi tulikuwa hotelini.”
AUNT EZEKIEL
Kwa upande wake Aunt Ezekiel alitiririka: “Kwanza kabisa majibu yote ungekuwa nayo wewe (mwandishi wetu) maana kila dakika tulikuwa wote  na kila mtu unajua alilala na nani.
“Hao mapedeshee kama walikuwa wakizunguka hotelini ni juu yao lakini sisi tulienda kwa ajili ya kazi tu na si vinginevyo.
“Kuhusu nguo fupi, kwa upande wangu sioni kipya kwa sababu tangu nikiwa mdogo ndiyo nguo zangu.
“Siku zote mtu akisema nguo zangu ni za kujiuza, hana jipya tena ni mzushi wa hali ya juu.”
Mastaa hao wakiwa stejini ndani ya Triple A.
WEMA
Alipotafutwa ‘mama lao’, Wema aliwaka: “Huyo aliyesema hayo mambo ni mpuuzi. Kwanza mawazo yangu yalikuwa hayawazi huo upuuzi kabisa.
“Akili yangu yote ilikuwa kwenye shoo tu maana nilikuwa nawaza itafanikiwa au vipi na ndiyo maana imefana kama ulivyoona.
“Tangu nilipofika hotelini nilikuwa nikilala na Kajala hadi siku naondoka maana tulikwenda na kitu kimoja kwa nini tujichanganye na vitu vingine visivyokuwa na manufaa kwetu?
“Kwa sasa nimetulia na mtu wangu, niende kuhangaika na mapedeshee wa nini?
“Mbona hakuna nafasi hiyo kwa sasa? Mavazi yangu ni ya kawaida siku zote.”

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate