MADIVAS wa Bongo Movies, Wema Sepetu, Kajala Masanja na Aunt Ezekiel wamenaswa wakishindana uzuri wao kuanzia kwenye midomo hadi katika uwezo wao wa kukata mauno.
Uwanja wa ‘mashindano’ ulikuwa ni pande za
Arusha walipokwenda kwa ajili ya kumtambulisha msanii anayepiga mzigo
kwenye lebo ya Wema, Endless Fame, Miraji Hussein ‘Mirror’.
Weekly Star Exclusive ilishuhudia tukio zima ambapo mastaa hao
walianza kufanya vituko hivyo ndani ya Hotel ya Point Zone iliyopo
jijini hapo, kamera ya paparazi wetu iliwamulika wakishindana kumpata
staa mwenye mdomo mzuri kuliko wenzake.Waligusanisha vichwa na kisha kujitazama katika kioo kisha kuanza kutambiana huku kila mmoja akidai yeye ndiyo mkali kuliko mwenzake. Hawakuishia hapo, walisimama na kuonesha uhodari wa kukata mauno na kudai wataumalizia mpambano huo katika Ukumbi wa Tripple A.
“Mnanionaje? Nataka kujua nani zaidi katika yetu hapa au ngoma droo nataka kujua hilo jamani? Kama hapa droo, kivumbi zaidi ni huko ukumbini,” alisika Wema.
Mastaa hao walipofika katika Ukumbi wa Triple A, waliendeleza mpambano huo ambapo mashabiki walipagawa na kutoa maksi kwa kupiga kelele za shwangwe kila walipokuwa wakikatika huku wakimwagiwa noti.
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment