EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, March 14, 2014

AIRTEL YAKABIDHI MILIONI 50 KWA MSHINDI WA PROMOSHENI YA MIMI NI BINGWA LEO


Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya hundi kwa Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto). Pembeni ni Meneja Masoko wa Airtel , Upendo Nkini.
Meneja Masoko  wa Airtel , Upendo Nkini (kushoto) akikabidhi hundi kwa Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto). Pembeni ni  kushoto ni rafiki wa mshindi huyo Antidius Diocresi.
Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto) akiongea kushukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuweza kuanzisha promosheni hiyo ambayo imeweza kumfanya akawa bingwa. Pembeni ni  Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando.
Kampuni ya simu za mkononi ya kupitia promosheni yake ya mimi ni bingwa  iliyomalizika hivi karibuni imemkabidhi mshindi wake BW, Rashidi Kagombora mkazi wa Bukoba hundi ya shilingi milioni 50 leo katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel tunawashukuru wateja wote walioshiriki kikamilifu katika promosheni yetu ya MIMI NI BINGWA, leo tunamkabidhi bw, Kagombola kitita chake kupitia hundi hii ya mfano na baada ya siku chache pesa zake zitaingia katika akaunti yake ya benki moja kwa moja”

Vilevile tunafuraha kuwatangazia kuwa jumla ya wateja 14 wa Airtel walioshiriki katika promosheni ya MIMI BINGWA wataondoka kesho kwenda nchini Uingereza jiji la Manchester CITY na watapata nafasi ya kushuhudia soka LIVE kati ya Manchester United na Liverpool siku ya jumapili tarehe 16/03/2014 soka litakalochezwa saa 9 na nusu alasiri.
Washindi wa MIMI NI BINGWA wanaotarajiwa  kuondoka kesho siku ya ijumaa ni GEOFREY DAVID MSITU, JOSEPH STEVEN MAMBO,SEVERA MORIS MATHIAS, HARRSON WILSON, RAFAEL WAIRES KABENGA, EDMUND HENRY KAGIMBO, AMINIYEU NLILIE NATAI, MAULID BARAKA KITENGE, JOSEPH MOSES NDOSSI, CHARLES JOSEPH BUCHWA, GOODLUCK RICHARD KIMARO, RAHABA EUSEBIUS MVUONI, RAJAB SAID MANGARA, na watasindikizwa na  Meneja Masoko wa Airtel Bi UPENDO GILLIARD NKINITunatoa  pongezi kwa washindi wote walioibuka na zawadi mbalimbali  kupitia promosheni hii iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu. Pia tunawapongeza wateja wengine wote walioshiriki katika promosheni lakini hawakushinda ikumbukwe kuwa hii ni bahati nasibu hivyo kila mtu anajishindia kwa bahati yake

Nae  mshindi wa Promosheni hiyo Bw, Rashidi Kagombola alisema “ninafurahi sana kuwa mshindi wa mamilioni haya, kwa kweli namshukuru sana mungu kwa kuniwezesha kubadili maisha kwa haraka hivi, leo hii natoa ahadi kwa Airtel na watanzania wenzangu kuwa nitahakikisha nazitumia kwa uangalifu pesa hizi ili kukuza biashara yamgu ya samaki”
Promosheni MIMI BINGWA imekwisha huku jumla ya pesa taslim milioni mia tatu ishirini na nne 324 zikiwa zimekwenda kwa wateja toka mikoa na sehemu mbalimbali, vile vile jumla ya washindi wengine 35 wamepata zawadi ya nafasi yakusafiri na kwenda Uingereza katika jiji la Manchester na watalipiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na gharama za malazi, usafiri, pamoja na gharama zote za kuandaa safari hadi kupatikana kwa hati ya kusafiria na VISA ya kwenda Uingereza na kushuhudia SOKA katika kiwanja cha OLD Traford cha Mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate