MOblog
Tanzania hivi karibuni ilifanya mahojiano na Mjasiriamali na mbunifu wa
mavazi nchini Doreen Noni aliyehudhuria mkutano wa Uchumi Duniani
uliofanyika huko Davos, Uswisi (World Economic Forum) mwezi uliopita juu
ya yote anazungumzia nafasi ya Wanawake, Vijana na Ujasiriamali
endelea…….
MOblog:
Ulipata nafasi ya kuhudhuria mkutano wa Uchumi duniani (World Economic
Forum 2014) hebu tueleze ulipata vipi nafasi ya kuhudhuria?
Doreen:
Mimi nilipata nafasi ya kuhudhuria (World Economic Forum) kupitia
asasi ya Global Shapers ambayo ni delegation ya vijana kupitia World
Economic Forum na vijana kuanzia miaka 20 mpaka 30 ambao kazi yao kuu
ni kuangalia vijana ambao wanaleta mabadiliko katika jamii na ushiriki
wa vijana katika maeneo mbalimbali, ya ujasiriamali kwa hiyo nilituma
maombi kwenye jukwaa la Uchumi Duniani na wao wakaona nafaa kuhudhuria
na nikahudhuria kwa hiyo nikawa mjumbe wa World Economic Forum kama
kijana na jukwaa la kuwakilisha vijana wa bara la Afrika na nimehudhuria
mikutano mitatu ya uchumi duniani mpaka sasa.
MOblog: Je kwenye mkutano huu wa hivi karibuni nini kilijitokeza?
Doreen:
Nilikuwa kwenye session tofauti nilikuwa kwenye panelist mbalimbali,
kama vile Innovation and Design na panelist nyingine ilikuwa Africa the
next billionaire ambayo kulikuwa na marais mbalimbali kama vile Goodluck
Ebele Jonathan; Rais wa Nigeria, Aliko Dangote; Afisa Mtendaji Mkuu wa
Dangote Group na John Mahama; Rais wa Ghana, hii session ilikuwa
inaogelea kuhusu umati wa watu Afrika na vijana tulikuwa kama 50 ambao
tulihudhuria mkutano huu na vijana wengi Afrika wanatuma maombi duniani
na kila session wanataka vijana wahudhurie kwa hiyo wanataka kujua uwezo
wa vijana katika maswala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kijamii.
Kusoma Mahojiano yote Ingia hapa
No comments:
Post a Comment