EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, March 15, 2014

HATIMAYE JOHARI KUOLEWA!

KILA jambo na wakati wake! Hatimaye staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ yuko kwenye mwanga wa maisha ya ndoa kufuatia Kiongozi wa Kundi la Mtanashati, Ostaz Juma Namusoma kuweka wazi uhusiano wao wa kimapenzi huku akisema ana mpango wa kumuoa kabisa, Risasi Jumamosi linakupa zaidi.

Staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
YAMEKUJAJE?
Hivi karibuni katika mtandao wa kijamii wa Instagram, Ostaz alitumbukiza picha inayomwonesha yeye akiwa katika ‘pozi nono’ na Johari huku akimsifu mwandani wake huyo. Hali hiyo ilisababisha maswali kwa baadhi ya mashabiki wa Johari.
Risasi Jumamosi lilianzia hapo kuchimba hatua kwa hatua na kubaini kuwa, wawili hao wako ‘klozidi’ tangu kitambo hasa baada ya penzi bubu la Johari na staa mwenzake wa sinema za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuparaganyika.
Kwa sasa Ray anadaiwa kutoka kimapenzi na mcheza filamu mwenzake, Chuchu Hans ambapo nao inadaiwa wako katika mikakati ya kufunga ndoa kama si pingu za maisha.

Johari na Ostaz Juma katika picha ya pamoja.
Chanzo chetu kimoja kilisema kuwa, Ostaz amekufa kimapenzi kwa Johari, ‘hakohoi, hanywi maji, halali usingizi’ na yuko tayari kwa ndoa itakayokuwa ya kifahari.
“Ukitazama hapo Johari hana kipingamizi, ingekuwa zamani angesema yuko na Ray kuna kikwazo cha yeye kuolewa na Ostaz, lakini kwa sasa kipi kitamzuia?” chanzo hicho kilipayuka.

Ray na Chuchu Hans wakiwa katika pozi la kimahaba.
MSIKIE OSTAZ
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo na picha ya wawili hao kwenye mtandao, mapaparazi wetu walimsaka mwanaume huyo kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kupitia simu yake ya mkononi na mambo yalikuwa hivi:
Risasi Jumamosi: Kaka kuna tetesi kwamba una uhusiano na Johari, unasemaje?
Ostaz: We nani?
Risasi: Mwandishi wa Risasi Jumamosi.
Ostaz: Ndiyo Johari ni wangu na mimi ni wake, tutafunga ndoa watu watashangaa sana.
Risasi Jumamosi: Huoni kama Ray atakukasirikia?
Ostaz: Kwani yeye ndiyo amemzaa Johari?
Risasi Risasi: Lakini kaka wewe mbona umeoa?
Ostaz: Mbona sikuelewi, Muislam mwisho ni wake wangapi?
Risasi Jumamosi: Vipi mkeo karidhia na lini ndoa?
Ostaz: Na Johari anataka kuslimu kuwa Muislam, tumepanga jina, ataitwa Rahma.
Risasi Jumamosi: Jambo jema. Mmeanza lini uhusiano wenu?
Ostaz: Hayo mengine muulize Johari mwenyewe mi nimeshasahau maana nina mambo mengi ya kujenga taifa.
“Lakini mimi nilianza na Johari kabla ya huyo Ray wenu, wakati huo Johari akiwa anaishi Mburahati (Dar), yeye alikuwa anafanyia mazoezi ya kuigiza pale TZF (baa), Kigogo.”
JOHARI SASA
Kutokana maelezo hayo ya Ostaz, Risasi Jumamosi lilimtafuta Johari kwa simu yake ya mkononi na kumuuliza kama kweli yu mapenzini na mfanyabiashara huyo maarufu jijini Dar.
Johari: “Hamna bwana, kama Ostaz mwenyewe ndo’ kasema hivyo huenda alikuwa anatania tu. Kweli hakuna kitu kama hicho, ila ni mtu ambaye nina ukaribu naye mkubwa lakini si mapenzi.
Risasi Jumamosi: Kama ametutania mbona sisi siyo watani wake?
Johari: Mimi sijui sasa, yeye ndiyo anajua.
Risasi Jumamosi: Kama ni hivyo, wewe huoni kwamba utani wake ni mkubwa sana?
Johari: Mimi sijui chochote jamani, muulizeni yeye.
Baada ya kuzungumza na Johari, Risasi Jumamosi lilimgeukia Ostaz na kuulizwa kama kuna utani ndani ya maelezo yake.
“Jamani, ninyi mnachotakiwa kukielewa ni kuwa, Johari ni wangu na mimi ni wake. Siku ya ndoa tutaitangaza, itakuwa ndoa kubwa sana na Johari nitamfanyia mapenzi ambayo hajawahi kufanyiwa tangu azaliwe.”
 WASEMAVYO MASTAA KUHUSU JOHARI NA OSTAZ
Baada ya kumalizana na wawili hao, Risasi Jumamosi liliwatafuta mastaa wa filamu za Bongo ili kusikia kutoka kwao wanachokijua kuhusu Johari na Ostaz.
Mastaa waliopatikana ni watatu, lakini wote walitoa ushirikiano kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini.
WA KWANZA, MWANAUME:
“Khaa! Mbona siyo siri, kwani nyie mmejua lini? Wale wako tangu zamani sana tena wengine mpaka tukadhani walishaachana, kumbe bado wapo pamoja?”
WA PILI, MWANAUME:
“Oohooo! Mlikuwa hamjui? Wale ni wapenzi. Mimi ninavyojua wana mpango wa kufunga ndoa lakini sijui ni lini na Johari atabadili dini.”
WA TATU, MWANAMKE:
“Mh! nilishasikiasikia, unajua Johari ni msiri sana, hajawahi kuweka wazi lakini ni kweli wana uhusiano wa kimapenzi.”
KAMA NI KWELI, CHEKI SINEMA YAKE
Endapo ni kweli Johari atabadili dini, ina maana atakuwa amekwenda sambamba na Ray kwani yeye anadaiwa kubadili dini kwa ajili ya kumuoa Chuchu Hans, Johari atabadili dini ili aolewe na Ostaz!
CHANZO NI GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate