Gwiji la sanaa nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’ akiwa nyumani kwake Tabata-Mawenzi, jijini Dar.
Akizungumza na paparazi wetu nyumbani kwake Tabata-Mawenzi, jijini
Dar, Mzee Small alisema ugonjwa huo uliomuanza tangu Mei, mwaka 2012,
umemsumbua kiasi cha kushindwa kufanya shughuli zake za kawaida kwani
alikuwa ni mtu wa kushinda ndani.“Sikuwa nikiweza kutembea, kwa zaidi ya miaka miwili nilikuwa mtu wa kulala kitandani tu, nikitaka kuelekea chooni mke wangu ndiye aliyekuwa akinisaidia,” alisema Mzee Small.
Mzee Small akiwa na mke wake nyumani kwake Tabata-Mawenzi, jijini Dar.
Akiendelea kufunguka, Mzee Small alisema anawashukuru baadhi ya
wasanii ambao walikuwa pamoja kwa kumpa misaada mbalimbali lakini pia
aliwazungumzia wale ambao wamemtenga kipindi chote cha kuugua.“Ninaposikia wasanii wanasema kwamba kuna umoja, napinga hilo. Kuna watu wengi nimefanya nao kazi na hata wengine kuwatoa mikoani na kuja Dar kwa ajili ya kufanya kazi, wakafanikiwa lakini sikuwaona katika kipindi chote cha kuteseka kwangu kitandani,” alisema Mzee Small na kuongeza:
“Kuna ambao wamejitoa kwa hali na mali, wapo wengi siwezi kuwataja wote lakini wanajijua nao niwashukuru sana akiwemo msamaria mwema mmoja ambaye amenilipia gym nafanya mazoezi, hadi sasa naendelea vizuri.”
Mzee Small ameahidi kurudi tena katika uwanja wa maigizo kwa kutoa filamu kadhaa mwaka huu kwani anajiona kuwa na nguvu za kufanya kazi tena.
“Nitarudi. Wale walioanza kunisahau nawaambia kwamba nitarudi tena na kutoa kazi nyingi zenye mafundisho,” alisema Mzee Small huku akisimama na kuanza kutembea kujipa mazoezi.
CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment