Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita utakumbuka nilizungumzia suala la
kuwajali wapenzi wetu. Niligusia suala ya kuwapa nafasi watuchune.
apo
walioshituka kuona kichwa kile cha habari lakini kiukweli sikumaanisha
kuchuna kule ambako wanawake micharuko hufanya hasa kwa waume za watu,
nilimaanisha utayari wa kila mmoja kumsaidia mwenzake kifedha. Mkeo
akitaka pesa ili aende saluni kama zipo, mpe! Akihitaji pesa akanunulie
vipodozi na nguo kama pesa zipo, mpatie.
Tusibaniane pale ambapo Mungu ametujaalia uwezo wa kuwafanya wenza
wetu waonekane watu mbele ya wenzao. Hili ni kwa mke na mume na hata
wapenzi wa kawaida. Baada ya kugusia hayo, nigeukie sasa kwenye mada
yangu ya wiki hii.
Ndugu zangu, nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya
wanawake wakielezea kukerwa kwao na tabia za waume zao kuendekeza sana
tendo la ndoa. Wanaume wanaoweka mbele suala hili husimamia kwenye ile
pointi kwamba, kufanya mapenzi na wake zao kila wanapojisikia ni haki
yao ya ndoa.
Hali hii imewafanya baadhi ya wanawake kufikia hatua ya kuomba talaka
kutoka waume zao kutokana na kushindwa kuhimili vishindo. Wanaume wengi
huwa wagumu sana kuzitoa talaka na ndiyo maana wakati mwingine wanawake
hulazimika kwenda mahakamani kudai talaka japo si wote wanaodai kwa
kukimbia tendo la ndoa.
Wanaoendelea kuwepo kwenye ndoa na wanaume wanaohusudu mapenzi,
hulazimika wakati mwingine kujifanya wanaumwa ili kuepukana na kero hii.
Kimsingi ndoa haiwezi kunoga bila kuwepo suala la kukutana faragha na
hili linaelezwa hata kwenye vitabu vya dini.
Tunaponyimana licha ya kuwakera wenza wetu lakini pia tunamkasirisha
Mungu ambaye anatutaka tufanye hivyo ili tuzaliane. Hata hivyo, kila
kitu kina kipimo chake na kikizidi inakuwa ni tatizo. Wazungu wanasema;
‘Too much is harmful’.
Hili lipo hata kwenye suala la mapenzi. Ukiwa kila wakati utataka
kukutana na mpenzi au mwenza wako faragha, hata ile raha iliyotarajiwa
haiwezi kupatikana, matokeo yake itakuwa ni karaha. Nalazimika kuandika
makala haya kutokana na ukweli kwamba, huko mtaani kuna baadhi ya watu
wameliweka sana mbele suala hili.
Yaani wao kila wakati ni mapenzi… mapenzi…mapenzi….Usiku kucha
hawataki hata wenzao wapumzike. Ni mchakamchaka mwanzo mwisho. Sasa huku
ni kukomoana au kitu gani? Wengine wapenzi wao hawajisikii kufanya
tendo hilo kutokana na kuumwa au kutokuwa na hamu.
Hiyo ni hali ya kawaida kwa binadamu lakini utashangaa mwanaume
anakuja na kulazimisha mambo. Huku ni kuumizana na raha haiwezi
kupatikana kwa njia hii. Katika lile tendo furaha inapatikana pale kila
mmoja anapokuwa anajisikia kuwa faragha na mwenzake.
Ni tendo takatifu linalohitaji maandalizi ya kimwili na kifikra kwa
hiyo tusipelekeshane. Wakati mwingine tuzikontroo hisia zetu. Katika
hili naomba nishauri yafuatayo; Kwanza tujitahidi sana kujitoa kwenye
kundi la watu wenye pepo wa ngono. Tukiwa kwenye kundi hili, si kwa
mwanaume tu bali hata kwa wanawake ni lazima tutakuwa ni watu wa kuwaza
kufanya mapenzi kila wakati.
Tuwe watu wa kuzishughulisha akili zetu kwa kufanya kazi na kuwaza
mambo ya kimaendeleo na si kila wakati kutaka kuwa na wapenzi watu
faragha. Itaendelea wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment