| Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo akizungumza kabla ya pambano hilo. |
| Mmoja wa mabondia waliopambana katika mapambano ya utangulizi akitokwa mchuzi baada ya kuchezea masumbwi toka kwa Bondia Mwakipesile. |
| Bondia Mwakipesile(Shoto) akisukuma konde . |
| Hatimaye bondia Mwakipesile akaibuka mshindi kwa pointi |
| Likafuata pambano la Bondia Massawe toka kibosho . |
| Akapambana na Bondia Rasta toka jijini Arusha. |
| Bondia Rasta akachezea ngumi za kutosha toka kwa Mkibosho.Masawe. |
| Bondia Rasta akaomba Poooo.akasalimu amri akasema siendelei na pambano taumia. |
| Bondia Masawe toka Kibosho akapewa Ushindi kwa kumtwanga KO Bondia Rasta. |
| Bondia Rasta akifurahia ushindi. |
| Likafuatia pambano kali tena na hapa ni kati ya Fredy George kutoka Himo mwenye Bukta ya njano na Pascaly Bruno wa Moshi. |
| Ngumi zikapigwa kwa raund zote nne. |
| Mabondia wote wakiwa hoi kama anavyoonekana Fredy George akivuliwa Groves. |
| Bondia Pascaly Bruno akatangazwa mshindi . |
| Baadae sasa likafuata pambano lililokuwa likisubiriwa na wengi ni la kuwania mkanda wa taifa kati ya Bondia Alibaba Ramadhan na Roy Mbunda. |
| Bondia Alibaba Ramadhan akiingia ukumbini akiwa anasindikizwa na wapambe wake. |
| Bondia Alibaba akipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa pambano. |
| Pambano likaanza ndani ya round ya pili tu Bondia Alibaba anasukuma konde kwa bondia Roy Mbunda lililompeleka chini. |
| Baadae Roy Mbunda akaamka akigugumia maumivu ya mguu akidai msuli wa paja umebana. |
| Mwamuzi wa pambano hilo Said Chaku akalazimika kutaka kufahamu endapo Mbunda ataendelea ama la. |
| Mwamuzi Chaku akalazimika kukatisha pambano kutokana na Bondia Mbunda kuda hatoweza endelea na pambano. |
| Roy Mbunda akisikilizia maumivu. |
| Maumivu yakamzidi Roy Mbunda na kuanza kuangua kilio. |
| Mashabiki nao walilipuka kwa kelele. |
| Hatimaye madaktari ikawalazimu kuingia ulingoni kutoa huduma ya kwanza kwa Roy Mbunda. |
| Akanyooshwa viungo. |
| Bondia Alibaba Ramadhan akatangazwa bingwa wa taifa . |
| Kisha akavalishwa mkanada wake wa Ubingwa akapata picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi pamoja na wadhamini. |
| Ngumi iliyompelleka chini Roy Mbunda ilisababisha pia uharibifu wa kamba za Ulingo na hapa ni baada ya bondia Mbunda kudondokea . |
| Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Kilimanjaro Elikunda Kipoko pamoja na wadhamini wakifurahia ushindi wa Alibaba. |
| Akapongezwa Roy Mbunda. |
| Akapongezwa Alibaba kwa ushindi na sifa aliyoupatia mkoa wa Kilimanjaro. |
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment