EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, April 8, 2014

RAIS KIKWETE APONGEZWA

Bw. Stanley Bergman akiteta jambo na Balozi Manongi wanaonekana pia wageni waalikwa waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla hiyo.
Rais na Mwanzilishi wa MCW, Bw. Eddie Bergman akielezea historia ya Taasisi hiyo ambayo aliianzisha ( 1999) akatumia fursa hiyo kutoa shukrani zake kwa wadau , wafadhili na marafiki mbalimbali ambao wameendelea kuiwezesha Taasisi hiyo na hatimaye kupitia kwayo kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali na uwezeshaji wa vijana.
Bw. Stanley Bergman, Mwenyekiti na CEO, Henry Schein Inc akizungumza wakati wa hafla ya miaka kumi ya uchangiaji wa Taasisi ya Miracle Corners of the World ( MCW) ambayo pia imetimiza miaka kumi na tano ya kuanzishwa kwake, katika mazungumzo yake alitoa shukrani na pongezi kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa namna ambayo amekuwa akishirikiana na Taasisi hiyo ambayo inaendesha shughuli hususani uboreshaji na uimarishaji wa huduma ya afya ya kinywa.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akisema machache wakati wa hafla hiyo.
Sehemu ya wageni waalikwa, aliyekaa mstari wa mbele ni Bw. Ali Velshi ambaye alikuwa ndiye mshereheshaji wa hafla hiyo. Bw. Velshi ni mtangazaji maarufu wa vipindi vya Biashara katika Televisheni ya CNN hivi sasa amehamia Al Jazeera Amerika
Balozi Manongi akiwa na Mwanamziki Maarufu Kanda Bongo Man, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kanda Bongo Man alikuwa mmoja wa wageni waalikwa na kama alivyo Balozi Manongi naye pia ni Mwenyekiti wa Heshma wa MCW.

Na Mwandishi Maalum

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,  ameelezwa  kuwa ni kiongozi ambaye amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwa  Taasisi  zisizokuwa  za  kiserikali na hivyo kuchagiza kasi ya   taasisi  hizo kuwekeza katika miradi ya kijamii nchini Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na  Bw. Stanley Bergman,  Mwenyekiti na Mkurugenzi  Mtendaji wa Henry Schein Inc,  wakati wa hafla  ya miaka  kumi ya uchangiaji  wa shughuli za  Taasisi  ya Miracle Corners of the World ( MCW) hafla iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanziswa kwa  Taasisi hiyo  yenye  makazi yake Jijini New York, nchini Marekani.

Hafla hiyo  ilifanyika usiku wa Jumatatu na kuhudhuriwa na wageni wa kada  mbalimbali  yakiwamo makampuni makubwa  kama vile  NASDAQ OMX, CITI  na  the UPS Foundation ambayo yamekuwa yakichangia shughuli za  Taasisi  hiyo.  

Miongoni mwa wageni waalikwa alikuwa ni  Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi.

MCW  ilianzishwa mwaka 1999 na  Bw. Eddie  Bergman ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka kumi na  mitano, inajihusisha  miradi ya kijamii  ikiwamo ya huduma za afya, na uwezeshaji wa vijana na kukuza ushirikiano na  Taasisi nyingine.

Taasisi  hii  ilianza shughuli zake kwa kuanzisha kituo cha  vijana  jijini Arusha na baadaye  ikasambaza  huduma zake katika mikoa ya Iringa,  Dar es   Salaam, Ruvuma na Zanzibar.

“ MCW inajivunia  ushirikiano  na uhusiano wa karibu na Rais wa   Tanzania Mhe. Rais Jakaya Kikwete,  ambaye muwakilishi wake Balozi Manongi  yupo   pamoja nasi usiku huu. Ni ushirikiano na msaada wake wa hali na mali ndio  unaoifanya  MCW  iendele kutoa huduma zake nchini Tanzania. Napenda kutumia  fursa hii kumshukuru sana  Rais Kikwete”. Akasema.

Katika miaka  yake  15 ya  shughuli zake  hususani uwezeshwaji wa vijana  kutambua vipaji vyao vya uongozi na kubwa zaidi uimarishaji  na uboreshaji wa huduma ya afya hususani afya ya  kinywa.  MCW imekuwa ikishirikiana   kwa karibu sana na Chuo  Kikuu cha Tiba na Sayasi  (MUHAS) katika  kuimarisha na  kuboresha Kitivo  cha Meno  kwa maana ya vifaa ,  mafunzo  na miundo mbinu.

 Ni katika hafla hiyo, ambapo  Rais na Mwanzilishi wa  MCW, Bw.  Eddie  Bergman wakati akielezea mafanikio ya  Taasisi  hiyo   alieleza kwamba  kontena lililokuwa na vifaa vyenye thamani ya dola za kimarekani 500.000 lilikuwa limewasili jijini  Dar es Salaam  ambapo kwa ushirikiano kati ya  Wizara ya   Afya na Ustawi wa Jamii na Bohari  Kuu ya  Madawa, ( MSD) kontena hilo limeshatolewa  bandarini na kukabidhiwa Chuo Kuu cha MUHAS.

Dkt. Marion Bergman ambaye  ni Mkurugenzi wa  miradi ya Afya katika  MCW alishuhudia kuwasili kwa kontena  hilo na makabidhiano.
Wakati wa hafla hiyo ya  jumatatu jumla ya dola za kimarekani 950,000 zilichangwa  kwa madhumuni ya kufanikisha shughuli za  Taasisi hiyo ambayo sasa  inazihusisha pia  Zambia,  Rwanda na  Sierra Leone.

Akizungumza  katika hafla hiyo,  Balozi Manongi,  alieleza kwamba Tanzania  imekuwa mmoja wa wanufaikaji wakubwa wa MCW  na kwamba  Tanzania itaendelea kuenzi  shughuli zake ambazo zimelenga katika kuinua na kuimarisha huduma za afya katika  maeneo ya pembezoni mwa Tanzania.


Baadhi ya  washiriki  waliopewa  fursa ya kuzungumza na ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na MCW walieleza kwamba kwa  kuja kwao  Tanzania  na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wadau mbalimbali wakiwamo vijana na wataalamu wa afya,  si tu kwamba wao wametoa, lakini  uzoefu walioupata katika maeneo waliyokwenda  umewabadili  kifikra na kimtazamo na kwamba wapo tayari wakati wowote kurejea  tena Tanzania.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate