BADO
hali ya huduma zinazotolewa na baadhi ya hospitali zetu nchini ni
mbaya, utendaji mbovu na wagonjwa hawajaliwi hata pale inapotokea
wamepelekwa wakiwa mahututi, Risasi Jumamosi linakufunulia.
Baada ya kuanika uozo wa hospitali kadhaa – za serikali na binafsi,
sasa kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global
Publishers, kilitinga katika Hospitali ya Wilaya ya Kinondoni, Palestina
na kugundua udhaifu mkubwa wa huduma mbovu zitolewazo hospitalini hapo.
YALITANGULIA MALALAMIKO
Wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti walipiga simu kwa OFMna kueleza namna hospitali hiyo inavyotoa huduma mbaya hasa Mapokezi, wauguzi na madaktari wa kitengo chote cha wagonjwa wa nje, ‘Outpatient Department’ (OPD).

OFM KAZINI
Aprili 23, mwaka huu saa 10:42 za alasiri, OFMwaliingia hospitalini hapo wakiwa tayari kwa kazi, ambapo mmoja wao alijifanya mgonjwa mahututi aliyehitaji huduma ya haraka.

Walipofika Mapokezi, pamoja na kuonekana mgonjwa kuwa na hali mbaya,
wahudumu hawakumpa kipaumbele na kuendelea kuwahudumia wagonjwa wengine
kwa foleni ambao hawakuonekana kuwa ‘serious’ sana.
Baada ya dakika 12 kupita bila msaada, mpelelezi mmoja wa
OFMaliyejifanya ni mwanafunzi mwenzake na mgonjwa, alikwenda dirishani
kuomba kuandikiwa kadi haraka ili aende kwa daktari, akapewa.
FOLENI NDEFU, HAKUNA DAKTARI
Mapaparazi wa OFMwakiwa na mgonjwa wao kwenye baiskeli ya wagonjwa, walifika kwenye foleni iliyokuwa na watu wengi wanaohitaji kuingia kwa daktari lakini hakuwepo ofisini kwake, zilipita dakika 14 ndipo akatokea.

Hata hivyo manesi waliokuwa wakirandaranda kwenye korido hawakutoa msaada wowote kwa wagonjwa waliokuwa wanamsubiri daktari.
MAIGIZO CHUMBANI KWA DAKTARI
Mgonjwa akionekana kuzidiwa sana (alipatia kweli kuigiza mgonjwa!) alimweleza daktari kuwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu makali mwilini, viungo kufa ganzi na shida katika mfumo wa upumuaji.

Hata hivyo, mgonjwa huyo alimweleza daktari kuwa hali hiyo ilimpata ghafla akiwa na wenzake chuoni, haikuwahi kumtokea kabla.
Baada ya kumpima shinikizo la damu, mgonjwa huyo alionekana yupo katika hali ya kawaida, kipimo kilisoma 110/70 mmHg.

TIBABILAVIPIMO
Katika hali ya kushangaza daktari huyo, bila kumpima mgonjwa ili kuthibitisha anachoumwa, aliagiza kwanza achomwe haraka sindano mbili – Diclofenac (ya maumivu) na Hydrocortisone (ya kutuliza maumivu ya kifua).

Kwa msaada wa wenzake, mgonjwa huyo alipelekwa chumba cha sindano na
kukubali kuchomwa sindano ya Declofenac kwa vile walijua ni ya maumivu
tu lakini wakagoma mgonjwa wao asichomwe ile nyingine mpaka watakapopewa
maelezo inatibu ugonjwa gani.
MAABARA
Baada ya kuchomwa sindano hizo alitakiwa kuelekea maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa vipimo mbalimbali ikiwemo cha malaria ambacho kitaalamu kiliandikwa RDT (Rapid Diagnostic Test for Malaria) na RPG.
Mapaparazi wetu walishuhudia wagonjwa wengi wakiwa kwenye foleni huku wengine wakiwa na hali mbaya kwenye baiskeli za wagonjwa wakisubiri huduma.

Paparazi wetu alilazimika kujilaza kwenye fomu katika foleni na
kusubiri hapo kwa takribani nusu saa ndipo alipochukuliwa vipimo na
kuletewa majibu baadaye yaliyoonyesha hakuwa na ugonjwa wowote.
Kwa kuwa kazi ilikuwa imeshakamilika, mapaparazi wetu hawakuona
sababu ya kurudi kwa daktari, walitokomea zao mitaani na mgonjwa feki
wao ambaye alionekana kuanza kupata nafuu.
MGANGA MKUU KIKAANGONI
Alhamisi, Aprili 24, mwaka huu, mishale ya saa 6:30 mchana, mmoja wa makachero wa OFMalifika hospitalini hapo na kuonana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina, Dk. Benedict Luoga ili azungumzie tuhuma hizo.

Baada ya kusikiliza madai hayo, Dk. Luoga alikataa kuzungumza kwa
maelezo kuwa yeye siyo msemaji, badala yake akamwelekeza mwandishi huyo
kwenda kwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Gunini Kamba
aliyedai ndiye msemaji.
No comments:
Post a Comment