EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, May 29, 2014

HATUJAWAHI KUMKOPESHA MBOWE, WALA KUWASAIDIA "SUGU" NA MSIGWA - MFUKO WA PENSHENI WA LAPF

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF NI MFUKO WA HIFADHI YA JAMII NCHINI TANZANIA WENYE MAKAO
MAKUU YAKE MJINI DODOMA.

MFUKO WA LAPF  UNAPENDA KUKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KUWA LAPF ILITOA MSAADA KWA MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEPH MBILINYI  (kulia) NA MBUNGE WA IRINGA MJINI MH. PETER MSIGWA (kushoto).

IELEWEKE KUWA INGAWA WAHESHIMIWA WABUNGE AU MTU AU TAASISI YEYOYE HAWAZUILIWI KUOMBA MSAADA WA KIJAMII, MH. MBILINYI NA MH. MSIGWA HAWAJAWAHI KUWASILISHA MAOMBI NA HAWAJAWAHI KUPEWA MSAADA WOWOTE NA LAPF.

AIDHA LAPF INAKANUSHA HABARI ZILIZOTOLEWA KATIKA GATEZI LA MTANZANIA LA TAREHE 26 MEI 2014 TOLEO NA. 7472 KUWA WAHESHIMIWA WABUNGE NI WASUMBUFU NA KUMFANYA MKURUGENZI MKUU ASIENDE BUNGENI.
LAPF INAKANUSHA PIA HABARI ILIYOTOLEWA KATIKA GAZETI LA THE GUARDIAN LA TAREHE 27 MEI 2014 TOLEO NA. 6031. IELEWEKE KUWA LAPF HAIJAWAHI KUMKOPESHA MH. FREEMAN MBOWE  (kulia) KIASI CHA SHILINGI BILIONI MOJA. MFUKO WA LAPF HAUNA UTARATIBU WA KUKOPESHA MTU MMOJA MMOJA HIVYO HAKUNA MIKOPO YA AINA HIYO. LAPF HUTOA MIKOPO YA WANACHAMA WAKE KUPITIA VYAMA VYA KUWEKA NA KUKOPA (SACCOS) NA MIKOPO YA NYUMBA KWA WANACHAMA WANAOKARIBIA KUSTAAFU.

AIDHA, SI KWELI PIA KWAMBA LAPF HAISHIRIKI KATIKA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU KWANI MFUKO HUU UKO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI NA INASHIRIKI KATIKA VIKAO HIVYO.

LAPF INAPENDA KUWAJULISHA UMMA WA WATANZANIA KUWA MFUKO HUTOA MISAADA YA KIJAMII KWA KUZINGATIA MPANGO NA BAJETI ILIYOIDHINISHWA NA KWA KUZINGATIA SERA YA MISAADA YA KIJAMII NA MAOMBI YANAYOWASILISHWA. PIA HAKUNA TAASISI AU MTU BINAFSI INAYOPEWA FEDHA TASLIM ISIPOKUWA MFUKO HUNUNUA VIFAA NA KUWASILISHA MOJA KWA MOJA KWA WAHUSIKA.

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UNAENDESHWA CHINI YA SHERIA
YA LAPF (THE LOCAL AUTHORITIES
PENSIONS FUND ACT NO. 9 OF 2006). SHERIA HII IMEFANYIWA MAREKEBISHO KUKIDHI MAHITAJI YA
SHERIA YA USIMAMIZI WA HIFADHI YA JAMII YA MWAKA 2008 (SSRA) NA KWA
SASA LAPF INAANDIKISHA WANACHAMA TOKA SEKTA ZOTE NCHINI NA JINA LA MFUKO
LILIREKEBISHWA NA SASA LINAJULIKANA KAMA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF (LAPF PENSIONS FUND).

SHUGHULI
KUU ZA MFUKO NI PAMOJA NA KUANDIKISHA WANACHAMA, KUKUSANYA MICHANGO, UWEKEZAJI
NA KULIPA MAFAO.

KWA SASA LAPF INATOA MAFAO MBALI MBALI AMBAYO NI MAFAO YA
UZEENI, MAFAO YA MIRATHI, MAFAO YA KUUMIA KAZINI, MAFAO YA UZAZI, MAFAO YA
KUJITOA, MSAADA WA MAZISHI, MIKOPO YA NYUMBA, MIKOPO YA WANACHAMA KUPITIA
SACCOS NA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUTOA MIKOPO YA ELIMU KWA WANACHAMA.

PAMOJA
NA MAJUKUMU MAKUU YA MFUKO YALIYOTAJWA HAPO JUU, MFUKO UNASHIRIKI PIA KATIKA
KUISAIDIA JAMII NA HIVYO KUSAIDIA KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI NA KUCHOCHEA
MAENDELEO ( CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY).

MISAADA
HII INA LENGO LA KUSAIDIA JAMII YOTE YA WATANZANIA YENYE MAHITAJI MBALI MBALI
NA KWA KUTAMBUA KUWA MISAADA HII ITAWANUFAISHA SI WANACHAMA WA LAPF TUU BALI
PIA WANANCHI WOTE.

LAPF
IMEKUWA IKITOA MISAADA YA KIJAMII KATIKA SEKTA MBALI MBALI KAMA VILE AFYA,
ELIMU, VITUO VYA WATOTO YA YATIMA, TAASISI ZA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM, SEKTA
YA MICHEZO NA KUSAIDIA MAAFA KWA KUTOA VIFAA MBALI MBALI KAMA  MASHUKA, VYANDARUA NA MADAWA, KATIKA ELIMU
KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA, UNUNUZI WA MADAWATI NA VIFAA VYA MAABARA. KATIKA
VITUO VYA WATOTO YATIMA LAPF IMEKUWA IKITOA MISAADA YA VYAKULA, MAVAZI NA VIFAA
VYA SHULE. KADHALIKA KATIKA MICHEZO LAPF IMEKUWA IKICHANGIA VIFAA VYA MICHEZO
KAMA JEZI NA MIPIRA.

KWA MIAKA MITATU MFULULIZO MFUKO WA LAPF NDIO UMEKUWA
MDHAMINI MKUU WA MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU (TUSA) AMBAO NI
WANACHAMA WATARAJIWA WA MFUKO.

KATIKA
MWAKA WA FEDHA 2013/2014 MFUKO WA LAPF UMETOA MISAADA MBALI MBALI KAMA VILE
VIFAA VYA UJENZI CHUO CHA MADAKTARI BUGANDO NA CHUO KIKUU HURIA (OUT).

KADHALIKA
LAPF IMEOTA VIFAA MBALI MBALI VYA SHULE KAMA VILE MADAWATI, TAA ZA SOLA NA
MASHINE ZA FOTOKOPI. 

KATIKA
SEKTA YA AFYA LAPF IMETOA MSAADA KWA HOSPITALI NA ZAHANATI MBALI MBALI NCHINI
KWA KUTOA VYANDARUA, MASHUKA, MADAWA, VIFAA VYA MAABARA, TAA ZA SOLA PAMOJA NA
KUCHANGIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI.

KATIKA
MICHEZO LAPF IMEENDELA KUWA MDHAMINI WA MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO
VIKUU (TUSA) NA VIFAA VYA MICHEZO KWA SHIRIKISHO LA SERIKALI ZA MITAA
(SHIMISEMITA).

HII
NI BAADHI TU YA MISAADA AMBAYO LAPF IMETOA KWA MWAKA HUU KWA KUZINGATIA MAOMBI
MBALI MBALI YALIYOWASILISHWA PAMOJA NA BAJETI NA MPANGO WA MFUKO ULIOIDHINISHWA.
KWA MWAKA HUU WA FEDHA, MISAADA YOTE HADI SASA INA JUMLA YA THAMANI YA SHILINGI
MILIONI MIA MOJA NA ISHIRINI. AIDHA, KUTOKANA NA UFINYU WA BAJETI YA MFUKO,
SEHEMU KUBWA YA MISAADA HII NI KATI YA SHILINGI LAKI TANO HADI MILIONI TATU.
MISAADA HII HUTOLEWA MOJA KWA MOJA KWA WALENGWA NA PIA SI FEDHA TASLIMU, BALI
VIFAA HUSIKA.
STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate