WACHEZAJI
wa Liverpool, akiwemo Luis Suarez usiku wa kuamkia leo walimwaga
machozi uwanjani baada mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Crystal
Palace iliyomalizika kwa sare ya kufungana mabao 3-3 ugenini.
Hadi
dakika ya 79, Liverpool walikuwa mbele kwa mabao matatu dhidi ya
Crystal Palace, pointi tatu zaidi ya Manchester City katika mbio za
ubingwa na kupunguza wastani wa mabao wanayozidiwa hadi kubaki sita.
Lakini
upepo ulibadilika na wakaambulia sare, hivyo sasa wanaizidi pointi moja
City wakiwa pia wamecheza mechi moja zaidi- maana yake ndoto za ubingwa
zimeanza kuyeyuka.
Hawezi
hata kutazama: Tegemeo la mabao la Wekundu wa Anfield, Luis Suarez
akisikitika baada ya mechi waliyoongoza kwa mabao 3-0 kwa zaidi ya robo
tatu ya mchezo, lakini wakamaliza kwa sare ya 3-3
Ganzi:
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard akiwa haamini macho yake baada ya
mechi na chini ni mshambuliaji Daniel Sturridge akiugulia maumivu pia ya
matokeo hayo.
Liverpool
ilipata mabao yake kupitia kwa Allen dakika ya 18, Sturridge dakika ya
53 na Suarez dakika ya 55, kabla ya Palace kuzinduka na kuchomoa haraka
haraka kupitia kwa Delaney dakika ya 79, Gayle dakika ya 81 na 88.
Hakika
ilikuwa huzuni kwa wachezaji wa Liverpool baada ya kushindwa kuondoka
na pointi zote tatu- maana yake sasa wana kazi ya kuhakikisha wanashinda
mechi zao zote zilizobaki, huku wakiwoambea dua mbaya wapinzani wao,
Man City.
No comments:
Post a Comment