EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, May 5, 2014

TUZO ZA KILI 2013/14: RIPOTI KAMILI

Stori: waandishi wetu
Mwisho wa ubishi! Hatimaye kile kinyang’anyiro cha Tuzo za Muziki za Kilimanjaro 2013/14 kimefikia tamati wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili ya matokeo na kilichojiri nyuma ya pazia.
Mshindi wa tuzo saba za KTMA Diamond akikabidhiwa tuzo na staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi 'Ray'.
NANI KASHINDA TUZO GANI?
Tuzo ya kwanza ilikuwa ni kipengele cha Wimbo Wenye Vionjo vya Asili vya Kitanzania ambapo tuzo ilikwenda kwa Bora mchawi wa Dar Bongo Massive.
...Akikabidhiwa tuzo na mchumba wake Wema Sepetu.
NI YOUNG KILLER
Tuzo ya pili ilikuwa ni ya Msanii Bora Chipukizi ambapo aliyeibuka mshindi ni dogo anayetokea Mwanza, Erick Msodoki ‘Young Killer’.
...Akipokea tuzo kutoka kwa George Kavishe.
CHEZEA JAYDEE?
Tuzo ya tatu ilikuwa kwenye Kipengele cha Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba, ngoma iliyoshinda ni Yahaya ya Judith Wambura ‘Lady Jaydee’.
...Akiwa na Nay wa Mitego baada ya tuzo yao ya Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana ambao ni Muziki Gani.
TAYARI DIAMOND KAKALISHA
Tuzo ya nne ilikuwa ni Kipengele cha Wimbo Bora wa Afro-Pop, tuzo ilikwenda kwa Ngoma ya Number One ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwaangusha Lady Jaydee, Abdu Kiba na Ali Kiba, Kassim Mganga na Rich Mavoko.
Shabiki wa Diamond akimpongeza kwa kutwaa tuzo nyingi.
Katika tuzo ya tano ilikuwa ni Kipengele Wimbo Bora wa Ragga ambapo Ngoma ya Nishai wa Chibwa akimshirikisha Juru.
Tuzo ya sita ilikuwa ni Kipengele cha Wimbo Bora wa Reggae ambapo Wimbo wa Na Wewe, mshindi alikuwa ni Dabo.

Weusi wakiwa na tuzo yao ya Kikundi Bora cha Mwaka, Kizazi Kipya.
MZEE YUSUF KATISHA
Katika tuzo ya saba, ilikuwa ni Kipengele cha Wimbo Bora wa Taarab, ngoma iliyoibuka kidedea ni Wasiwasi Wako wa Mzee Yusuf.
Msanii Bora wa Hip hop na Mtunzi Bora wa Mwaka Hip hop, Farid Kibanda 'Fid Q' baada ya kutwaa tuzo zake mbili.
JAHAZI KINARA
Tuzo ya nane ilikuwa ni Kipengele cha Kikundi cha Mwaka cha Taarab ambapo Jahaz Modern Taarab waliibuka kidedea.
Msanii Young Killer akipokea tuzo yake ya Msanii Bora Chipukizi Anayeibukia kutoka kwa msanii JB.
ISHA MASHAUZI NAYE
Katika tuzo ya tisa ilikuwa ni Kipengele cha Mwimbaji Bora wa Kike Taarab, mshindi alikuwa ni Isha Ramadhan ‘Mashauzi’.
...Killer akiwashukuru mashabiki.
MZEE YUSUF TENA
Kwenye Kipengele cha kumi ilikuwa ni Mwimbaji Bora wa Kiume Taarab ambapo kama kawa Mzee Yusuf aliibuka kinara ikiwa ni tuzo yake ya tatu.
Mwimbaji Bora wa Kike Bendi, Luiza Mbutu (katikati) akiwa na tuzo yake aliyokabidhiwa na wasanii kutoka Kenya, Amani na Kelvin Wyre.
KWELI USHAMBA MZIGO
Kipengele cha kumi ilikuwa ni Wimbo Bora wa Kiswahili Bendi, wimbo bora ulikuwa Ushamba Mzigo wa Mashujaa Musica.
Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi, Christian Bella akipokea tuzo yake kutoka kwa Issa Michuzi.
HONGERA DA’LUIZA
Tuzo ya kumi na mbili katika Kipengele cha Mwimbaji Bora wa Kike Bendi, tuzo ilikwenda kwa Luiza Mbutu wa The African Band ‘Twanga Pepeta’.
ASANTE JOSEE MARA
Katika kipengele cha kumi na tatu kilikuwa ni Mwimbaji Bora wa Kiume Bendi, tuzo ilikwenda kwa Josee Mara Bendi ya Mapacha Watatu akiwaangusha Chaz Baba, Kalala Junior, Khalid Chokoraa na Christian Bella.
FERGUSON HUREEE!
Tuzo ya kumi na nne ilikuwa katika Kipengele cha Rapa Bora wa Mwaka Bendi, tuzo ilikwenda kwa Saulo John ‘Ferguso’ wa Mashujaa Musica akiwaangusha Chokoraa, Kitokololo, Kanal Top na Totoo Zebingwa.
NI MASHUJAA MUSICA
Katika tuzo ya kumi na tano, kwenye Kipengele cha Bendi ya Mwaka, tuzo ilikwenda kwa Bendi ya Mashujaa Musica ikiwagaragaza Akudo Impact, Twanga Pepeta, FM Academia, Malaika Band na Mapacha Watatu.
LADY JAYDEE TENA
Tuzo ya kumi na sita ilikuwa ni Kipengele cha Mwimbaji Bora wa Kike Kizazi Kipya ambapo Lady Jaydee aliwagaragaza Vanessa Mdee, Linah na Maua.
Katika tuzo ya kumi na sana, ilikuwa ni Mwimbaji Bora wa Kiume Kizazi Kipya, mshindi alikuwa Diamond Platnumz akiwaangusha Ben Pol, Rich Mavoko, Ommy Dimpoz na Kassim Mganga huku akikabidhiwa tuzo hiyo na mpenziwe Wema Isaac Sepetu na kuibua makelele ‘oyooo...’.
ARUSHA ‘IN DA HOUSE’
Katika tuzo ya kumi nane, Kipengele cha Kikubi Bora cha Mwaka cha Kizazi Kipya, ushindi ulikwenda kwa Weusi kutoka Arusha ambao walikabidhiwa tuzo hiyo na aliyekuwa shemeji yao kwa memba mwenzao, Lord Eyez, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
VANESSA CHUPUCHUPU
Wimo Bora wa RnB, ushindi ulikwenda kwa Closer wa Vanessa Mdee huku viatu virefu chupuchupu vikitaka kumuumbua. Kwa upande wa Wimbo Bora wa Hip Hop, tuzo ilikwenda kwa Ngoma ya Nje ya Box wa Nikki wa Pili wa Weusi.
FID Q JUUU!
Katika Kipengele cha Msanii Bora wa Hip Hop, tuzo ilikwenda kwa Fid Q ambaye alizingirwa kila upande. Kwenye Wimbo Bora wa Kushirikiana, tuzo ilikwenda kwa Wimbo wa Muziki Gani aliomshirikisha Diamond Platnumz.
WATUMBUIZAJI
Awali kulikuwa na shoo za madasa mbalimbali kisha akafuatia Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na Bendi ya Motomoto.
EXTRA BONGO, TWANGA PEPETA
Baada ya hapo zilifuata burudani kutoka kwa Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ na Twanga Pepeta ambao kwa pamoja walionesha ‘lavu’ kwa kusalimiana.
WEUSI, MADEE
Baada ya dansi walipanda Weusi wakiongoza na Joh Makini ambao walivunja na ngoma yao kali ya Gere iliyowapandisha watu mizuka kisha kumpisha Hamad Ally ‘Madee’ akaburudisha kupitia ngoma yake ya Pombe Yangu.
Baadaye alipanda jamaa ‘mchaga’ Fredy Saganda ‘Mo’ na ngoma yake ya zamani ya Namna Gani kisha akaimba Wimbo wa Kiarabu na kusababisha ukumbi kurindima kwa shangwe na kutuza.
WASIOFIKA KUCHUKUA TUZO
Baadhi ya wasanii waliopata tuzo hawakufika kuchukua tuzo zao na badala yake walituma wawakilishi hivyo kula uso kuwa hawapendi kujumuika. Baadhi yao ni pamoja na Lady Jaydee na Mzee Yusuf. Kwa habari zaidi usikose Gazeti la Uwazi kesho Jumanne.
Imeandaliwa na: Musa Mateja, Shakoor Jongo, Gladness Mallya na Clarence Mulisa. 

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate