Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
KOCHA
Mbrazil Marcio Maximo, aliyekuwa kocha wa timu ya taifa (Taifa Stars),
muda wowote atatua nchini na kusaini mkataba wa kukinoa kikosi cha Yanga
katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na michuano ya
Kombe la Shirikisho barani Afrika, imefahamika.
Uongozi
wa Yanga katika mkutano mkuu wa dharura wa wanachama iiliofanyika
kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini hapa jana,
umesema umekuwa na mazungumzo ya muda mrefu na kocha huyo ili achukue
kandarasi ya kuinoa timu yao.
"Tunapenda
kuwaataarifu wanachama wa Yanga kwamba tuna mpango wa kumleta Maximo
kuifundisha timu yetu msimu ujao. Tumekuwa na mazungumzo naye kwa miezi
miwili sasa tukimwomba apungumze kidogo mshahara," amesema Yusuph
Manji, Mwenyekiti wa Yanga.
"Zoezi
la usajili linakwenda vizuri. Hatusajili wachezaji wengi kwa sababu
kikosi chetu cha msimu uliopita ni kizuri ndiyo tukaifunga hadi Al Ahly
ya Misri. Tunachokifanya kwa sasa ni kurekebisha maeneo ambayo tumebaini
kuwa na upungufu.
"Wachezaji
wote wanasajiliwa makao makuu ya klabu ili kuepuka matatizo ambayo
yamejitokeza huko nyuma," amesema zaidi kiongozi huyo.
Maximo,
raia wa Brazil aliiongoza Taifa Starsb kwa mafanikio makubwa akisifika
kama 'mhamasishaji' kutokana na Watanzania wengi kuingia viwanjani
kuiona timu yao ya taifa ikicheza dhidi ya timu mbalimbali.
Hamasa
ya Watanzania kuishangilia ilianza kupungua baada ya kuondoka kwa kocha
huyo na mikoba yake kuchukuliwa na Jan Poulsen ambaye baadaye arithiwa
na Mdenmark mwenzake Kim Poulsen aliyetimuliwa mwanzoni mwa mwaka huu.
Taifa
Stars kwa sasa iko chini ya Mholanzi Mart Nooij na Yanga haina kocha
mkuu baada ya kuondoka kwa Mholanzi Hans van der Pluijm Aprili mwaka
huu.
Aidha,
katika mkutano huo wanachama wamepitisha kuingizwa kwa kipengele katika
Katiba ya Yanga kinachotaka klabu hiyo iwe na Kamati ya Maadili kama
ilivyoagizwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka (TFF) Desemba
mwaka jana.
Kipengele
kilichopitishwa kinasema: "Kutakuwa na Kamati nya Maadili itakayokuwa
na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe watatu watakaoteuliwa na
Kamati ya Utendaji na muda wao hautazidi mwaka mmoja. Mwenyekiti lazima
na taaluma ya sheria."
"Kazi
za chombo hiki zitasimamiwa na Katiba ya Yanga na Kanuni za Maadili za
Yanga na endapo hazitajitosheleza, Kanuni za Maadili za TFF zitatumika
ipasavyo.
"Rufaa zote kutoka Kamati ya Maadili zitasikilizwa na Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF."
Aidha,
wakati Mwenyekiti wa Yanga akitengua kauli yake ya kutowania tena
uongozi, uchaguzi mkuu wa klabu hiyo sasa umepangwa kufanyika Juni 15
mwakani.
Wanachama
wa Yanga katika mkutano mkuu wa dharura wa marekebisho ya Katiba
kwenhye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini hapa leo,
wamekubaliana uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ambao awali ulikuwa umepangwa
kufanyika Juni 15 mwaka huu ufanyike mwakani ili kupishya shughuli
mbalimbali za maendeleo ya klabu hiyo ikiwamo marekebisho ya Katiba na
michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Novemba
mwaka jana, Manji alitangaza kutowania tena uongozi ndani ya klabu hiyo
ili kupisha watu wengine waiongoze klabu hiyo kongwe nchini katika kile
alichokieleza kuwa kutimiza matakwa ya demokrasia.
Lakini,
baada ya ajenda kuu ya mkutano mkuu wa jana kuingiza kipengele cha
kuunda Kamati ya Maadili ya Yanga kama ilivyoagizwa na Shirikisho la
Soka nchini (TFF) Desemba mwaka jana, wanachama wa Yanga katika kujadili
mengineyo waliamua kuwaondoa mkutanoni kwa muda wajumbe wa Kamati ya
Utendaji ya klabu hiyo ili kujadili kauli yao ya kutowania tena uongozi.
Baada
ya hoja hizo kujadiliwa huku wanachama mbalimbali akiwamo 'mzungu'
Javet Peytov mwenye kadi ya uanachama Na. 009472, wakisimama na
kuchagia, wajumbe hao walilazimika kufuta kauli hiyo na kurudhia kuwania
tena uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Atakuja? Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Marcio Maximo anatakiwa na Yanga SC |
No comments:
Post a Comment