Jina
la Tanzania linameremeta wakati wanamichezo wetu walipopita katika
maandamano ya ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye sherehe
kabambe za ufunguzi katika Uwanja wa Celtic Park jijini Glasgow,
Scotland, uliobeba watazamaji 40,000 huku watu bilioni 1 wakiangalia
live sherehe hizo kupitia katika TV zao. Takriban mashabiki 100,000, na
wanamichezo 4,000 kutoka katika nchi 71 zitakazoshindana wapo hapo kwa
michezo hiyo ambapo hii ni mara ya 20 kufanyika toka ianzishwe. Sehemu
ya wanamichezo wa Tanzania kwenye sherehe hizo za ufunguzi. Jumla ya
wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni
jitihada za Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini
kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali
wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za
Uturuki, China na New Zealand
Tanzania Oyeeeee....!!!!
Tanzania Oyeeeee....!!!!
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Suleiman Mjaya Nyambui (T-shirt ya njano) akihamasisha vijana wake
Nahodha na bondia wa Tanzania Seleman Salum Kidunda akipeperusha juu bendera ya Taifa wakati akiongoza wenzake kwenye maandamano hayo ya ufunguzi
No comments:
Post a Comment