KLABU za Liverpool na Barcelona zimefikia makubaliano ya biashara ya Luis Suarez jana usiku.
Kituo
cha Televisheni ta Katalunya kimeripoti kwamba ada ya uhamisho ya Pauni
Milioni 63 imekubaliwa na Suarez atasaini Mkataba wa miaka mitano,
ambao utamfanya awe mchezaji wa nne kulipwa fedha nyingi baada ya Lionel
Messi, Neymar na Andres Iniesta.
Liverpool wanaendelea na mipango ya kutaka kumsajili Alexis Sanchez wa Barcelona azibe pengo la Suarez.
Dili limetimia: Luis Suarez sasa yuko njiani kuhamia Barcelona.
Arsenal
inabakia kuwa chaguo la kwanza la Sanchez, lakini Manchester City na
United zimeonyesha pia nia ya kuitaka huduma yake sawa na Juventus.
Sanchez
atasafiri kutoka Santiago, Chile hadi Barcelona nchini Hispania
kujadili ofa hizo mezani. Barcelona inatarajiwa kutoa tamko rasmi juu
ya Suarez leo au kesho.
No comments:
Post a Comment