NYOTA wa Brazil, Neymar anaamini timu yake itashinda Kombe la Dunia bila ya kuwa na yeye.
Mchezaji huyo wa Barcelona aliaga mashineano hayo juzi usiku baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Colombia, Juan Zuniga.
Mchezaji
huyo ameelezea maumivu yake baada ya pogo hilo linalomuondoa Kombe la
Dunia mapema akiiacha timu yake imetinga Nusu Fainali- na zaidi
amewatakia heri wachezaji wenzake wabakize nyumbani.
Neymar
amesafirishwa kwa helikopta baada ya tiba ya awali kupelekwa Sao Paulo
kuanza mapumziko. Tayari FIFA imesema inalifanyia uchunguzi tukio hilo
kabla ya kumchukulia hatua Zuniga.
Neymar amesema bado anaweza kushangilia Kombe la Dunia na wachezaji wenzake mjini Rio
Safari njema: Neymar akipewa pole na Rais wa Shirikisho la Soka Brazil, Jose Maria Marin
No comments:
Post a Comment