Miss
Redd’s Shinyanga 2014 ni Nicole Franklyn Sarakikya (katikati) akiwa na
mshindi wa pili, Mary Emmanuely Bugingo na Mshindi wa tatu, Rachel
Mushi.
HATIMAYE Mkoa wa Shinyanga umempata mrembo atakayewakilisha Miss Redd’s Kanda ya Ziwa hivi karibuni,Mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Redd’s Shinyanga 2014 ni Nicole Franklyn Sarakikya [21] mrembo kutoka wilaya ya Kishapu.
Mshindi wa pili Mary Emmanuely Bugingo [20]kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ushetu akipata Shilingi 350,000/= na Mshindi wa tatu
Warembo wote 20 walipita jukwaani kwa kuonyesha mavazi ya ubunifu bila kusahau burudani iliyoporomoshwa na Mfalme wa Muziki wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati;Mzee Yusuf,Msanii Amani kutoka Kenya,MO Music pamoja na madansa machachari kutoka Kanda ya Ziwa.
Baada ya mchakato walitangazwa washindi walioingia Kumi bora,wakafuatiwa na tano bora wakiongozwa na Mary Bugingo,Rachel Mushi,Neema Kakimpa,Nyangi Warioba na Nicole Sarakikya.
Majira ya Saa Nane Usiku ndipo Jaji Flora Lauwo alimtangaza mwanadada Nicole kuwa Miss Redd’s Shinyanga2014,ukumbi mzima ulizizima kwa shangwe huku moja ya sifa iliyomuwezesha mwanadada huyo kutwaa taji hilo ni kujibu swali la ufahamu kwa makini zaidi akitumia lugha ya Kiengreza.
Kwa kutwaa taji hilo Nicole mbali ya kuuwakilisha mkoa nwa Shinyanga katika kinyang’anyiro cha Miss Redd’s Kanda ya Ziwa pia alipata Shilingi Laki Tano sambamba na Tarakilishi Mpakato {Laptop}yenye thamani ya Shilingi Laki Saba,huku mshindi wa pili Mary Emmanuely Bugingo [20]kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ushetu akipata Shilingi 350,000/= na Mshindi wa tatu akiibuka Mrembo kutoka Shinyanga Vijijini;Rachel Mushi [21] aliyepata kitita cha Shilingi 250.
Mshindi wa Nne Nyangi Warioba [22] kutoka Halmashauri ya wilaya ya Msalala na Mshindi wa Tano Neema Saimon Kakimpa [21] wa Kahama wote walipata kila mmoja Shilingi 150,000/= huku walioingia Kumi bora wakipatiwa kila mmoja Shilingi Laki Moja.
Aidha katika mchuano huo Mrembo Irine Ahmed Makwaiya kutoka tena wilayani Kishapu aliibuka kidedea kuwa Miss Vipaji 2014 na kujinyakulia kitita cha Shilingi Laki Tatu,baada ya kuwashinda wenzake;Nicole Sarakikya,Jacline Jackson, na Nilam Siraji Abdul.
No comments:
Post a Comment