Uzinduzi huo utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na tayari wasanii mbalimbali nchini wameshaalikwa kushiriki.
Rebecca
amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009),
Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at
Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits
(Januari 10, 2006).
Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo mpya ya Muhando ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook. Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.
Mbali
na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe
Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa,
Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.
No comments:
Post a Comment