EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, August 22, 2014

Basi lapigwa bomu

 IGP Mangu
Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, dereva wa basi hilo   namba   T 570 CBE, Benedict Emmanuel, alisema basi lake lilipigwa bomu jana saa 12:15 alfajiri   alipokuwa akitoka Kilelema kwenda mjini Kasulu.
“Kabla ya kupigwa bomu hilo, tulifika katika pori la Kasesema ambalo lina historia ya matukio ya uhalifu kwa kipindi kirefu.
“Tulipofika katika pori hilo lililoko Kilelema, niliona kwa mbali watu wawili wakiwa wamesimama barabarani. Kwa hiyo nilichokifanya, niliwawashia taa kali nikidhani ni watu wa kawaida.
“Mmoja kati yao, alikuwa mbele kidogo kwenye kona, nikaona kama ana silaha  lakini sikumjali sana, kwa hiyo nilijipa moyo ili niwapite kwa kasi.

“Wakati nikiendelea kuwafikiria watu hao, ghafla niliwafikia na hapo nikasikia mlio mzito kama wa bomu limepigwa nyuma ya basi upande wa kushoto.
“Yaani nilichanganyikiwa, nikataka kusimama, lakini abiria wangu wakasema ongeza spidi hao ni majambazi wametupiga bomu,” alisema Benedict na kuongeza:
“Nilikanyaga mafuta kwa nguvu nikafanikiwa kuwaacha mbali hadi nilipofika katika Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)   Migongo nikasimama.
“Nilipofika hapo kambini tukakuta abiria wawili wamefariki dunia na mmoja hali yake ilikuwa mbaya sana.
“Kwa hiyo, tulitoa taarifa kwa mkuu wa kambi hiyo ya jeshi naye akawapigia simu polisi ambao walikuja na taratibu za kuwapeleka majeruhi katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu zikafanyika,” alisema.
Kwa mujibu wa Benedict, eneo walipopigiwa bomu ni la hatari kwa kuwa wahalifu kutoka Burundi huteka magari ya abiria mara kwa mara.
“Eneo hilo ni la hatari kwa sababu Warundi wanafanya uhalifu mara kwa mara na wanapomaliza kufanya hivyo, wanarudi kwao kwa sababu hapo ni jirani sana na Burundi,” alisema.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kilelema, Benedicto Mahuta, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Buhigwe, SamwelI Utonga, alithibitisha kutokea   tukio hilo.
Alisema watu hao wanaosadikiwa ni majambazi, mara nyingi hutokea   Burundi.
“Ni kweli kuna basi   ya Hiace imepigwa bomu na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi kutoka Burundi.
“Eneo lilikotokea tukio hilo ni hatari kwa sababu matukio ya uhalifu yanatokea mara kwa mara na abiria huporwa mali kwa kutumia silaha.
“Lakini bado tunaendelea na upelelezi kuangalia namna ya kuwapata watu hao,” alisema Utonga.
Kwa muda mrefu Mkoa wa Kigoma umekuwa ni kati ya mikoa inayoripotiwa kuwa na matukio ya uhalifu wa kutumia silaha unaodaiwa kuhusisha raia wa nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Kutokana na hali hiyo, viongozi wa Serikali ya Tanzania na nchi hizo  wamekuwa wakikutana mara kwa mara  kujadili jinsi ya kukabiliana na wahalifu hao.
CHANZO: MTANZANIA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate