Madenti mambo vipi?
Naona maisha yanaendelea na kwa sisi mashabiki wa soka la Ulaya, msimu
wetu ndiyo umeshawadia. Hili soka la Bongo tunamuachia Malinzi na
wapambe wake wazidi kuliporomosha, sisi macho yetu kule Premiership, La
Liga, Bundesliga, Serie A, Ligue 1 na kadhalika.
Leo nina mada ambayo kwa kweli siwezi kuizungumzia kwamba eti enzi
zetu. Labda tu niseme kwamba wakati ule sisi tukisoma, teknolojia hii ya
sasa, ilikuwa ndiyo inaingia na kwa maana hiyo ilitupita.
Nazungumzia simu, kompyuta na zaidi mtandao wa Internet. Simu
tulitumia zile za mezani, yaani hadi urudi nyumbani au uende posta ndipo
unaweza kuwasiliana na mwenzako, lakini nao kwao wawe nayo.
Sasa nyinyi maanko mko kizazi cha Digitali, mnamiliki simu zenu za
mkononi, tena basi teknolojia ikiwa imewawekea kila kitu, yaani simu
lakini pia unaweza kupata internet inayokuingiza kwenye mitandao ya
kijamii ambayo inapendwa sana na vijana kama Instagram, Twitter,
Facebook, Viber, Tango, WhatsApp, YouTube na kadhalika.
Kwa kuwa sisi enzi zetu mambo haya hayakuwepo, siwezi kuweka
ulinganisho na ilivyo leo, lakini uzoefu nilionao katika mitandao hii,
unanifanya nijiulize kama tunaitumia kwa faida ya maisha yetu ya baadaye
au tunafanya ili kujifurahisha tu.
Internet ina faida nyingi sana kwenu, kwa sababu unaweza kujifunza
vitu vingi kama utapata mwongozo wa mwalimu kuhusu kitu chochote
duniani. Sisi tulio ofisini inatusaidia sana kupata taarifa za sasa hivi
zinazotokea popote. Hatupishani tena na habari kama ilivyokuwa zamani
tulipolazimika kusubiri magazeti ya siku hiyo ndiyo tujue kilichotokea
juzi.
Kule kwenye hiyo mitandao ya kijamii, vijana ni wengi na bila shaka
wanafunzi pia mpo wa kutosha. Ninaona baadhi yao wanatupia picha
wakionekana wapo bize kimasomo, ingawa inasikitisha kuona pia wengine ni
kama wanajiuza flan, kwa kuanika picha zao walizopiga wakiwa nje kabisa
ya mstari wa maadili.
Acha hiyo ya kujianika, lakini pia lingine linalokera ni jinsi
wanavyopigana vikumbo kutafuta marafiki wenye majina makubwa. Kila mtu
anataka kuwa friends na Diamond, Dimpoz, Wema, Kajala, Masanja
Mkandamizaji, Kidoti, Ray na mastaa wengine kemkem.
Sikatai, ni jambo zuri kuchat na marafiki, hasa kama hawa mastaa
wetu, lakini najiuliza kama hili ndilo jambo pekee tunalolifanya kupitia
mitandao hii. Maana kutwa utakuta madenti wanasimuliana jinsi Chris
Brown alivyomnanga Rihanna katika akaunti yake ya Twitter!
Siku hizi kuna hadi kutumiana picha kupitia simu zetu za mikononi,
wenyewe mnaita WhatsApp. Utawasikia, simu yako ina wazap? Nataka
nikutumie bonge la picha nipo beach jana nakula bata!
Nijaribu tu kuwashauri madenti ambao kwa vyovyote nyinyi ni baba na
mama watarajiwa, kwamba huu ni wakati mzuri sana wa kujaribu kutengeneza
maisha yetu ya kesho kupitia mitandao, hasa kwa mambo yanayohusu
masomo.
Zamani sisi tulikuwa tunasoma kitabu kimoja kiliitwa Jiandae, chenye
maswali mengi ya kila masomo tunayosoma. Sijui kama kipo siku hizi.
Kitabu hiki kilikuwa kinakusanya mitihani mingi ya taifa ya darasa la
saba iliyofanywa miaka ya nyuma yake, ili kumwandaa mwanafunzi kwa
mtihani wake wa kumaliza elimu ya msingi.
Lakini ninavyojua mimi, hivi sasa unaweza kujifunza au kupata
mitihani ya kidato cha nne ya mwaka jana kupitia internet. Ukajifua na
kujifua kuusubiri mtihani wako wa kidato cha nne au sita.
Ni bahati mbaya tu kwamba muda ukipita huwa haurudi, lakini nataka
niwaapie kuwa kama ndiyo ningekuwa denti sasa hivi kwa akili hizi na
teknolojia hii, mngenikamatia pale kwenye kile kibao cha HAKUNA SHULE
MBELE!
Saturday, August 23, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment