EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, August 14, 2014

JACK PATRICK HUKUMU NYEPESIII!

Stori: Imelda Mtema na Erick Evarist
 BAADA ya kushikiliwa kwa takriban miezi tisa kwa kesi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye Video Queen maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu ikawa ndogo zaidi, Amani linaibumburua habari kamili.
Jack Patrick wakati alipokamtwa.
HUKUMU NYEPESI? Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Jack, modo huyo alihukumiwa Jumatatu iliyopita (Agosti 11, mwaka huu) kwenye Mahakama ya Macau huko Hong Kong ambapo hukumu hiyo ilitofautiana na adhabu nyingine za madawa nchini humo ambazo huwa hukumu yake ni kunyongwa hivyo ya Jack kuonekana nyepesiii! KWA NINI NYEPESI?
Kikimwaga data, chanzo hicho makini kilidai kwamba, hukumu hiyo ya Jack ni nyepesi ukilinganisha na hukumu nyingine za madawa ya kulevya zinazotolewa nchini China ambapo hakimu alitumia muda wa dakika 27 tu kuisoma.

“Hukumu za madawa ya kulevya zinatofautiana nchini China. Kuna baadhi ya majimbo kama Beijing huwa wao ikithibitika umebeba madawa ya kulevya, unanyongwa lakini baadhi ya maeneo unafungwa miaka kadhaa. Miaka hutofautiana kulingana na sheria walizojiwekea,”
kilifunguka chanzo chetu. HUKUMU YA JACK IPOJE? Ilidaiwa kwamba, kwa mujibu wa hukumu hiyo aliyohukumiwa mrembo huyo, anaweza kupunguziwa muda wa kifungo kulingana na nidhamu atakayoionesha gerezani kama mahakama ilivyoelekeza.
Madawa aliyokamatwa nayo.
“Anaweza akapunguziwa kifungo kwa sababu hukumu imeeleza wazi kwamba anaweza kupunguziwa adhabu hiyo kama atatimiza masharti ya kinidhamu ambayo sheria za China zinamtaka atimize,” kilisema chanzo hicho.
TUJIUNGE NA CHANZO “Amehukumiwa juzi Jumatatu, ametakiwa kwenda jela miaka sita, nilikuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara lakini juzi hiyo ndiyo kanitumia taarifa kwamba amehukumiwa na kunieleza kwamba siku hiyo aliduwaa kwa muda maana hakuamini kama anaweza kuhukumiwa kwani alikaa muda mrefu bila kujua hatima yake,” kilisema chanzo hicho kilicho karibu na Jack.
JACK AFURAHIA HUKUMU! Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya hukumu hiyo kupitishwa, Jack alifurahia hususan kuwepo kwa kipengele cha uwezekano wa kupunguziwa kifungo kama atakidhi masharti aliyopewa na mahakama.
“Baada ya kutafakari kwa kina hukumu yake, Jack anaonekana kuifurahia kwa sababu anaamini kwake yeye itakuwa ni rahisi kutimiza masharti ya kuwa mstaarabu kadiri kipengele hicho kilivyomuelekeza,” kilisema chanzo. NDUGU HAWAJUI LOLOTE? Katika hatua nyingine, chanzo hicho kilifunguka kuwa ndugu wa Jack waliopo Bongo hawakuwa na taarifa zozote kuhusiana na hukumu hiyo.
Video queen Jack Patrick akipozi.
Kilisema kuwa kwa upande wake iliwezekana kupata haraka taarifa hizo kwani alikuwa akiwasiliana na Jack mara kwa mara kwa njia ya barua. “Ilikuwa ni rahisi mimi kunipa taarifa hizi haraka kwa sababu nilikuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara, labda sasa hivi kwa kuwa nawapa ninyi (waandishi wetu) hizi taarifa ndiyo wanaweza na wao kujua kinachoendelea,” kilisema chanzo hicho.
NDUGU WASAKWA Wakati gazeti hili linakwenda mtamboni, lilifanya jitihada za kuwatafuta ndugu wa Jack waishio jijini Dar lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda kwani namba zao za simu zilikuwa hazipatikani.  Hata hivyo, rafiki wa karibu wa familia ya Jack ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini alisema wamezipokea habari hizo kwa furaha kwani kulikuwa na hofu kubwa kuwa huenda ndugu yao akanyongwa.
“Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na Jack wameipokea hukumu hiyo kwa furaha maana walikuwa wakihofia adhabu ya kunyongwa ambayo inatolewa zaidi nchini China,” alisema rafiki huyo wa familia.  JUX NAYE Ili kuzidi kujiridhisha zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta rafiki wa karibu wa Jack ambaye alikuwa akitajwa kuwa mpenzi wake, Juma Khalid 'Jux Vuitton' lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.
CHANZO GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate