EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, August 14, 2014

WAKATI PHIRI AMETUA DAR, ANGALIA LOGA ALIVYOIAGA DAR ES SALAAM




Wakati Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri raia wa Zambia ametua nchini, angalia aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Zdravko Logarusic alivyoliaga jiji la Dar.


Kupitia mtandao wa Facebook, Loga ametupia picha mbili huku akiandika “by by Tanzania), akimaanisha bye bye Tanzania.

UONGOZI wa Simba umeamua kumfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Zdravko Logarusic, lakini kocha huyo ameondoka na kitita cha Sh56 milioni kwa muda wa wiki tatu pekee tangu aliposaini mkataba mpya klabuni hapo bila kufanya kazi yoyote ya maana.
Logarusic amechukua kitita hicho akiwa ameiongoza Simba kwenye mechi moja tu ya kirafiki dhidi ya Zesco ya Zambia ndani ya muda huo ambapo Simba ililala kwa mabao 3-0.
Kwanza Julai, 22 mwaka huu, kocha huyo alisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kukinoa kikosi hicho cha Simba ambapo alichukua Dola 24, 000 (Sh 39.7 milioni) za ada ya kusaini mkataba huo.
Pili kocha huyo alipokea mshahara wa mwezi mmoja aliofanya kazi ambao ulikuwa ukamilike wiki ijayo na pia amepokea mshahara wa mwezi mmoja wa bure ili kuvunja mkataba wake.
Hivyo kocha huyo amepokea jumla ya dola 10,000 (Sh 16.5 milioni) za mishahara yake ya miezi miwili klabuni hapo. Jumla ya fedha hizo ni Sh56milioni.
Mbali na fedha hizo alizoondoka nazo, kocha huyo aliiongoza Simba kushika nafasi ya pili ya Kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu. Simba ilitinga fainali ya michuano hiyo ambapo ilipoteza kwa bao 1-0 mbele ya KCCA ya Uganda.
Katika rekodi nyingine Logarusic aliiongoza Simba katika mechi 13 za Ligi Kuu Bara, Simba ilishinda mara tatu pekee.
Ilipoteza michezo mitano na kutoka sare mitano na kumaliza nafasi ya nne. Logarusic aliikuta Simba katika nafasi hiyo hiyo ya nne wakati anakabidhiwa timu Desemba mwaka jana kwa mkataba wa kwanza.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate