EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, August 31, 2014

MKOA WA KAGERA WACHUKUA TAHADHARI DHIDI YA EBOLA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe akitoa ufafanuzi namna Serikali livyojipanga kukabiliana na ugonjwa wa Ebola mkoani humo kwa  kuongeza vifaa kinga na kuwawezesha kielimu  wataalam wa afya wanaofanya kazi ya uchunguzi wa dalili za ugonjwa huo walioko katika vituo vya ukaguzi mpakani.
Afisa Afya wa Kituo cha Ukaguzi cha Kabanga, mpakani mwa Tanzania na Burundi  Bw. Amos Mangaluke akipitia fomu zilizojazwa na raia kutoka nje ya nchi wanaotumia mpaka huo kufuatia  zoezi la uchunguzi wa dalili za awali za ugonjwa wa Ebola linalofanyika kituoni hapo.

Ofisi ya Uhamiaji ya Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi.
Kizuizi cha magari katika mpaka wa Kabanga unaotenganisha Tanzania na Burundi, wilayani Ngara.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO
31/8/2014, Kagera
MKOA wa Kagera umechukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola  kwa kuongeza nguvu katika udhibiti na ukaguzi wa raia wa kigeni kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaoingia nchini Tanzania kupitia vituo vya mpakani vya mkoa huo.

Akizungumza katika mahojiano maalum wilayani Ngara, Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe amesema kuwa kufuatia hali hiyo serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeongeza vifaa kinga na kuwawezesha kielimu  wataalam wa afya walioko katika hospitali za mkoa huo na vituo vya ukaguzi mpakani.

Amesema kuwa mkoa huo kijiografia unapakana na nchi tatu zikiwemo Uganda kwa upande wa Kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi na kuongeza kuwa mkoa kupitia kamati za Afya na wataalam wa afya walioko maeneo yote ya vituo vya ukaguzi wanafanya kazi zao ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa kila anayeingia nchini kupitia vituo hivyo anachunguzwa dalili za Ebola.

“Mkoa wa Kagera kama tunavyojua unapakana kwa karibu sana na nchi za Burundi, Rwanda na Uganda, kuna mwingiliano mkubwa sana wa watu kutoka eneo moja kwenda jingine hapa lazima tuchukue tahadhari kubwa , ninawahakikishia wananchi kuwa  tumejipanga vizuri katika kuimarisha uchunguzi kupitia kamati zetu za afya” Amesisitiza.

Amesema kufuatia uwepo wa ugonjwa huo katika nchi ya jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uongozi wa mkoa kupitia kamati ya Afya na ile ya Ulinzi na Usalama unaendelea kuwaelimisha wananchi kupitia vituo vya mbalimbali vya radio vya mkoa huo kuhusu dalili za ugonjwa huo , namna ya kujikinga na namna ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo watabaini mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.

Kwa upande wake Afisa Afya wa Kituo cha ukaguzi cha Kabanga, mpakani mwa Tanzania na Burundi  Bw. Amos Mangaluke akizungumzia hali ya ukaguzi wa raia wanaoingia nchini kupitia mpaka huo amesema kuwa  zoezi la uchunguzi wa dalili za awali za ugonjwa wa Ebola linafanyika kwa ufanisi mkubwa kufuatia kituo chake kuwa na vifaa kinga vinavyomsaidia wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema takribani watu 500 wanaotumia  mpaka huo wa Kabanga huchunguzwa afya zao kwa siku ambapo hujaza fomu maalum ya taarifa  ambayo hutumiwa na wataalam wa afya kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate