EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, August 15, 2014

NUHU, SHILOLE YANAKUJAJE KIZAZI HIKI?

BAHATI mbaya sana, simjui huyu bwana mdogo, anayekwenda kwa jina la Nuhu Mziwanda, aliyekuwa rafiki wa kiume wa msanii anayekimbiza katika muziki wa mduara, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole.
Naambiwa naye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, ingawa sijawahi kuisikia kazi yake yoyote. Lakini nikiri kuwa nimeiona picha yake mara nyingi, akiwa na mpenziwe na hata na watu wengine. Ni kijana mtanashati anayeweza kuwavutia wasichana wanaopenda mabrazamen!

Kwa muda mrefu, Nuhu na Shilole walikuwa wakiishi pamoja kama mtu na mpenzi wake. Mara kadhaa, yamewahi kuibuka madai kuwa kijana huyo alikuwa ni mdogo kiumri kwa msichana, lakini mara zote, mkali huyo wa kibao cha Paka la Baa amekuwa akikataa.
Binafsi aliwahi kuniambia wanaosema umri mdogo wa mpenzi wake, ni wambeya, wanamuonea wivu, kwa sababu yeye ana umri sawa na mwenzake. Haina ubishi kwamba walipendana na ili kuwathibitishia watu hivyo, Nuhu alijichora tatoo kwenye paja la mkono wake, akiwa ameandika maandishi yanayosomeka Shishi Baby, jina lingine la kisanii la Shilole!
Lakini katika hali isiyotarajiwa, penzi la Shilole na Nuhu likaparanganyika ghafla. Ni hapa ndipo ninapotaka kujikita leo ninapozungumza na huyu bwana mdogo. Najua, umri wake bado mdogo, hivyo kuna mambo mengi kwake ni mageni na asiyo na uzoefu nayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tatoo aliyojichora Nuhu, ni ile ambayo haiwezi kufutika, kwa maana hiyo pamoja na kupigwa kibuti, Shishi Baby itaendelea kung’ara mkononi mwake na kila siku ataiona.
Moja kati ya vitu ambavyo mtu anapaswa kuviogopa na kuwa na tahadhari kubwa kabisa ni mapenzi, hasa haya ya kizazi cha sasa chenye kupenda kuiga, anasa, utanashati na kulelewa (Shugamami na shugadadi).
Mapenzi yamesababisha wengi kuharibu maisha yao na kama mnavyojua, watu wanauana kila siku, mke au mume anamuua mwenzake, tena wakati mwingine, kikatili kabisa. Mapenzi ya siku hizi yanahitaji ‘timing’. Uaminifu, siyo tu ule wa kutotoka nje ya ndoa, bali kupendana kwa dhati ya moyo, haupo.
Watu wanapendana kulingana na upepo unavyokwenda, leo wanashibana sana, kesho chui na paka.
Hatukatai kuonyeshana mapenzi, tunawaona watu ufukweni kila siku wameshikana viuno, wanakulana denda hadharani na wakati mwingine hata zaidi ya hapo. Ni wakati wao, unaruhusu kwa sababu ni nyakati za furaha. Kesho wakigombana, kukumbatiana kwao jana ufukweni hakuonekani.
Kwanza, utamaduni wa kujichora tatoo binafsi huwa siupendi kwa vile naamini siyo wetu, ni wa kuiga. Lakini kama ni kuongeza mapambo mwilini kwa kuwa wao ni wasanii, zipo tatoo za kujichora kwa rangi, badala ya hizi za kutoboa mwili. Siku ikikuchosha, unaitoa.
Halafu, nadhani kama ni kujichora kuonyesha mapenzi kwa mtu, watu pekee wenye hadhi hiyo ni watoto wako, mama au baba yako. Hawa, vyovyote itakavyokuwa, hata mgombane vipi, bado watabaki kuwa ni damu yako.
Nasisitiza tena, kila mtu ana haki ya kupenda atakavyo, lakini jambo moja muhimu ambalo nina uzoefu nalo, mapenzi ya enzi hizi za dotcom ni ya upepo. Kuna machungu mengi ambayo yanawafanya watu kujutia uamuzi wao wa kuoa au kuolewa na walionao sasa. Wakati mababu zetu walizeekea kwenye ndoa, asilimia chache sana ya vijana wa sasa wanaoweza, angalau kukaa miaka kumi katika ndoa.
Sidhani kama kweli Nuhu alimpenda kihivyo Shilole na kama ndivyo, nimpe pole na kumtahadharisha asije chora tena tatoo nyingine ya mwanamke mwilini mwake, wanaume wenzake watamcheka!

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate