Magari yakipita katika
barabara ya Moshi Bar - Mazizini ambayo mkandarasi wake Controlled
Blusting inayojenga barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe urefu wa
Kilometa 3 imerundika vifusi kwa muda mrefu sasa bila kuvisambaza jambo
ambalo limekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Inadaiwa kuwa inapaswa
tangu kumwaga kwa vifusi hivyo hadi kusambazwa isizidi siku 28 lakini
vifusi hivi vimesha pita muda huo na dalili ya kusambwazwa hivi karibuni
haipo kwani mkandarasi huyo hata vifaa vyake vya kazi havipo katika
eneo la kazi jambo ambalo linazidishisha hofu kwa watumiaji wa barabara
hiyo ambayo baada ya kungwanguliwa hivi sasa imesheheni vumbi na mchanga
kusumbua baadhi ya maeneo.
No comments:
Post a Comment