EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, September 3, 2014

DIAMOND MARUFUKU UJERUMANI

Stori: Sifael Paul na mitandao/Global Publishers
Kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili iliyopita baada ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart, Ujerumani, mwanamuziki huyo anadaiwa kupigwa marufuku kutia maguu nchini humo.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
SHUHUDA WETU
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini mjini humo, ambacho pia kilikuwepo ukumbini wakati vurugu zilipoibuka, uchunguzi wa awali umeonesha kwamba, gharama ya vitu vilivyoharibiwa inakadiriwa kuwa zaidi ya Euro 128,322 sawa na Sh. milioni 280.

Viti vya ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart, Ujerumani vilivyoharibiwa na mashabiki waliopoteza uvumilivu kusubiri shoo ya Diamond Platinum.
“Tukio la vurugu za Diamond limeripotiwa kwenye magazeti tofauti mjini hapa lakini kubwa ni hasira ambayo mashabiki wa Diamond wameionesha waziwazi.
“Kwa mfano Gazeti la Stuttgarter la leo (Jumatatu) la mjini hapa limeandika:
Gari la polisi likiwasili eneo la tukio kutoa Msaada.
‘MASHABIKI WANA HASIRA NA DIAMOND’.
Kwenye habari zao waliwahoji watu waliofurika ukumbini hapo.
“Wengi walikuwa wakilalamika kwamba walikata tiketi mapema kwa euro 25 (zaidi ya Sh. elfu 55) kwa kichwa. Yaani kuanzia saa 4:00 watu walikuwa tayari wanamsubiri Diamond.
MUDA WAYOYOMA
“Kuna muda DJ alitangaza kwamba angepanda stejini kuanzia saa 6:00 usiku hivyo watu wakapunguza hasira. Cha ajabu saa saba ilikatika, nane ikapita, tisa ndipo mtiti ukaanza.
Mashabiki wakilizingira gari la Diamond.
“Sasa hebu fikiria mtu umetoa buku 55 yako halafu hadi saa tisa usiku mtu haonekani! Hapo ndipo tatizo lilipoanzia!” yamesomeka hivyo magazeti ya hapa.Ilisemekana kwamba ilipofika saa 10:00 alfajiri ndipo Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake, raia wa Nigeria anayejiita Kamabritts.
CHUPA ZARUSHWA
Mashabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki huyo na promota wake.Ilidaiwa kwamba kilichowakera zaidi mashabiki hao ni vyombo vibovu vilivyofungwa ukumbini humo kitu ambacho kiliwafanya kuvunjavunja viti, meza, jukwaa na vyombo vya muziki kisha kusababisha watu kujeruhiwa na hasara kubwa ya mamilioni ya shilingi.
Mapolisi wakilinda gari la diamond dhidi ya mshabiki waliokuwa na gadhabu.
MAJERUHI WAONGEZEKA
Baadhi ya vyombo vya habari mjini humo, juzi (Jumatatu) viliripoti kuongezeka kwa majeruhi wakiwemo MaDJ wawili ambao hali zao bado ni tete hospitalini kwa sasa.
Katika vurugu hizo, DJ mwanamke aliyetajwa kwa jina la DJ Flor alizimia hivyo akakimbizwa hospitalini huku mashabiki wakimpa kipigo DJ Drazee.
KAULI YA POLISI
Polisi eneo la Sindelfingen, Stuttgart nchini Ujerumani walisema tukio hilo ni la aibu hivyo uchunguzi wa kina unaendelea ambapo promota huyo na Diamond watalazimika kulipa vitu hivyo na kwamba hawatawaruhusu kufanya tena shoo eneo hilo na kwingineko nchini humo.
Magari ya wagonjwa yakiwa tayari kuhudumia majeruhi eneo la tukio.
Vyombo vya habari vya Ujerumani viliandika kuwa polisi wamesema walitenga askari 18 wa kutuliza ghasia ambapo walifyatua mabomu ya machozi ili kumuokoa Diamond.Walisema kwamba kitendo cha msanii kuchelewa kufika jukwaani nchini humo ni kitu cha hatari mno kwani mashabiki wanaheshimu muda wao.
PROMOTA ASAKWA
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni polisi walikuwa wakimsaka promota huyo, Kamabritts ili wamalizane na Diamond aruhusiwe kuondoka nchini humo na asirudie tena jambo kama hilo.
MCHEZO NYUMA YA PAZIA
Duru za kiuchunguzi zinaonesha kwamba, shoo nyingi za wasanii kutoka Afrika zinazofanywa kwenye kumbi mbalimbali katika baadhi ya nchi za Ulaya, hucheleweshwa makusudi ili vinywaji viuzike.
'Mzee wa Mdogomdogo', Diamond Platinum taratiiiibu akiondoka eneo la tukio huku gari likishambuliwa na washabiki wenye gadhabu.
Ilidaiwa kwamba, katika tukio hilo baya, kulikuwa na tatizo la kiusimamizi kwani mbali na promota, menejimenti ya Diamond ilipaswa kuwa na ratiba kamili na siyo kumsikiliza promota ambaye anawaza zaidi kuingiza kipato kuliko heshima ya msanii hivyo jamaa huyo kuwa staa wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kusababisha vurugu Ulaya.
LAWAMA KWA MENEJA WA UJERUMANI
Kuna maelezo kwamba, Diamond huwa ana mameneja wengi kwenye kila nchi anayokwenda hivyo huyo meneja wa Ujerumani alistahili lawama zote kwani alipaswa kujua kinachoendelea ukumbini.
BABU TALE ANASEMAJE?
Kuhusu hilo, Risasi Jumatano lilimtafuta meneja wa Diamond ambaye hakusafiri na msanii huyo, Babu Tale na kuulizwa kulikoni yaliyomkuta Diamond Ujerumani ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kweli inasikitisha lakini haukuwa mpango wa Diamond. Ninachojua alikuwa akimsikiliza promota.
Ni changamoto kubwa lakini tunaomba radhi kwa mashabiki wetu wa Ujerumani. Next time wampokee vizuri.“Lakini kwa upande mwingine unajua ni jambo kubwa na niseme tu kuwa ukilitazama tukio hili kibiashara ni kama limemkuza zaidi kujulikana duniani. Umeona ameripotiwa na vyombo vingi vya habari. Mitandao ya kijamii ndiyo usiseme. Yote kwa yote tumejifunza na tunaomba radhi. Tusiangalie tulipoangukia, tuangalie tulipojikwaa.”

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate