EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, September 3, 2014

JOTI, LULU BALAA

Stori: Waandishi wetu
Mastaa wawili Bongo waliokuwa watangazaji wa Shindano la Kuibua Vipaji vya Kuigiza, Tanzania Movie Talents (TMT), Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Lucas Mhuvile ‘Joti’ wamezua balaa na kuwaacha hoi mashabiki waliohudhuria fainali za shindano hilo kufuatia aina ya viwalo walivyokuwa wamepigilia.
Staa wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiingia ukumbini na kigauni kilichoacha sehemu kubwa ya kifua wazi.
Mpango mzima ulijiri kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, wikiendi iliyopita ambapo katika kuonesha ubunifu, mchekeshaji Joti, alitupia vazi la jinsi zote ambalo upande mmoja lilionekana ni sketi ya kike na mwingine suruali ya kiume.

Kama hiyo haitoshi, mwili wake aliugawa katika nafsi hizo mbili kwani licha ya sketi, pia mguu wake wa kushoto alivaa kiatu cha kike, kama ambavyo kichwani kwake, alisuka nywele upande mmoja kama mdada.Kitendo hicho kilionekana kama kuwapa bichwa wanaume wenye kufanya mapenzi ya jinsia moja, kwani waliona ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kuvaa mavazi ya kike.
Staa wa vichekesho Bongo, Lucas Mhuvile ‘Joti’ akitumbuiza jukwaani ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
Kwa upande wake, Lulu alivaa kivazi kilichoonesha sehemu kubwa ya mwili wake, kikiwa kimeziba matiti kwa mbali na kusababisha wanaume wakware kutokwa na udenda.
Katika fainali hizo za kumsaka mwenye kipaji cha kuigiza ukumbini hapo, mshiriki kutoka kusini mkoani Lindi, Mwanaafa Libuyu ndiye aliyeibuka mshindi na kuondoka na cheki ya Sh. milioni 50.
LULU AINGIA UKUMBINI
Shushushu wetu alimshuhudia Lulu akizama ukumbini humo akiwa amevalia gauni hilo lililoacha wazi sehemu ya mwili wake hivyo kujichafua mbele ya mamia ya mashabiki waliohudhuria.
“Yaani Lulu huwa anaonekana kama hajali vile, hebu muone nguo aliyovaa, imemuacha wazi sana, karibu mwili mzima uko wazi na anatangaza kwa kujiamini mpaka dah! Ni balaa!” alisikika mmoja wa wahudhuriaji hao.
‘Joti’ akizidi kuwaonyesha vimbwanga vya 'kikomedi' watazamaji waliohudhuria fainali za TMT ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
Kwa upande wake, Lulu alionekana kujiamini kupita kiasi bila kujali macho ya watu kwani alifanya kazi yake vizuri na hakuwa na wasiwasi wowote kufuatia nguo aliyokuwa ameivaa mwanzo.
JOTI NAYE
Kufuatia kipaji alichonacho, Joti, kila mtu hakuamini pale alipopanda stejini kutumbuiza kwa staili ya aina yake kufuatia vazi lake alilokuwa amevalia yaani nusu mwanaume na kuwafanya watu washindwe kukaa na kuishia kuangalia shoo aliyokuwa akiitoa kwa mashabiki.
“Ama kweli watu wana vipaji vyao, yaani kwa wakati mmoja Joti ameweza kuigiza kama mwanamke na mwanaume. Ukiachana na hayo, hadi nguo nayo imeshonwa hivyo! Dah! Fundi alifanya kazi tena nampongeza sana Joti maana nilijua anakuja kuigiza,” alisikika mhudhuriaji mwingine.
Mshiriki wa TMT kutoka kusini mkoani Lindi, Mwanaafa Libuyu akishangilia ushindi alioupata.
Katika maelezo yake, Joti alisema sababu ya kufanya vile ni sapraizi tu kwa mashabiki wake kwani huenda walijua atakuja kama ambavyo huwa anafanya sehemu mbalimbali.
“Nimeamua kuja kivingine, hii staili ni ya kawaida tu, sema watu wameshangaa kuniona vile, ndiyo maana Lulu alisema ni sapraizi kwa mashabiki, ni kweli nimewafurahisha sana na huwa wanashindwa kunielewa kwa jinsi ninavyobadilikabadilika,” alisema Joti.
Mwanaafa Libuyu akikabidhiwa zawadi.
Joti hakuishia hapo kwani baada ya mshindi kutangazwa tu, alitoa shoo ya nguvu huku watu wakimzunguka na kumuimbia kwa kufurahishwa jinsi alivyokuwa akicheza.
Kabla ya shindano hilo, Lulu na Joti waliwahi kudaiwa wanatoka lakini kwa pamoja walikanusha vikali skendo hiyo na kuweka hadharani kuwa uhusiano wao ni wa kikazi tu.
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate