Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Roho inauma! Kwa mara nyingine, kaburi la aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Rachel Leo Haule ‘Recho’ (pichani) limeloa machozi ya mastaa wakati wa kusimikwa msalaba baada ya kujengwa na kuonekana la kisasa, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.
Mchungaji akiongoza ibada ya kubariki na kuutakasa msalaba utakaowekwa kwenye kaburi la marehemu Recho Haule.
Katika tukio hilo lililojiri wikiendi iliyopita, vilio vya mastaa
vilianzia Kanisa la Anglikana lililopo Magomeni-Mwembe Chai, Dar ambapo
ilifanyika ibada maalum kwa ajili ya kumuombea marehemu huyo na wengine
waliotangulia mbele ya haki.
Ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu Recho wakifuatilia ibada ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Magomeni-Mwembe Chai, Dar.
Ibada hiyo iliyoambatana na kuombewa na kutakaswa kwa msalaba huo,
iliongozwa na Mchungaji Mtweve na baadaye walielekea Makaburi ya
Kinondoni, Dar lilipo kaburi alilopumzishwa Recho.Walipofika makaburini, mastaa hao walijikuta wakiangua vilio huku baadhi yao wakizimia kwa kumkumbuka mpendwa wao.
Tofauti na mastaa wengine, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Blandina Chagula ‘Johari’ walipitiliza kwa kulia kwa sauti kubwa.
Kuna wakati Odama alishindwa kuvumilia kulisogelea kaburi kwani aliangua kilio kilichosababisha mama wa Bongo Muvi, Herieth Chumila kumzuia kwa kuhofia kuishiwa nguvu.Mwisho, Odama na aliyekuwa mchumba wa Recho, Saguda George walitoa neno la shukrani kwa watu wote waliofika eneo hilo na kuomba ushirikiano kwa lolote litakalotokea.
Nayo familia ya Recho, iliwapongeza Odama na Saguda kwa kuwa na moyo wa upendo kwa marehemu tangu alipoumwa mpaka alipoaga dunia hadi kumjengea kaburi na kuwaomba waendelee kushirikiana kwa ajili ya umoja waliounganishwa na Recho.
Mbali na Odama, Johari, Herieth na Saguda, baadhi ya mastaa wengine ni pamoja na Steve Nyerere, Mike Sangu, Najma, Lamata, Kupa na wengine kibao.Recho (26) alifariki dunia Mei 25, mwaka huu wakati ajikifungua ambapo kichanga chake nacho kiliaga dunia.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment