EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, September 2, 2014

MUME ASIMULIA ALIVYOFANYIWA USODOMA

Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa MH! Hatimaye yule mwanaume aliyedaiwa kufumaniwa na mke wa mtu na hatimaye kufanyiwa usodoma na  watu sita, akiwemo mume wa mwanamke huyo amefungukia mchezo mzima.
Mwanaume aliyedaiwa kufumaniwa na mke wa mtu na hatimaye kufanyiwa usodoma.
Hivi karibuni mwanaume huyo (jina tunalo) ambaye ni mume wa wake wawili na mkazi wa Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala jijini Dar mwenye umri wa miaka 34 alikutwa  na mkasa huo kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Yombo Executive inayomilikiwa na Athuman Maembe (pichani).
 
Mmoja wa watuhumiwa wanaoshikiliwa na polisi kuhusiana na kesi hiyo.
Mara baada ya picha za tukio hilo kuenea kwenye mitandao ya kijamii na watu kushangaa, gazeti hili lilituma timu yake ya habari za uchunguzi ili kupata ukweli wa tukio hilo.Uwazi lilifanikiwa kumpata mwanamume huyo ambaye ni mfanyabiashara, pia alijitambulisha kuwa yeye ni mwelimishaji rika wa magonjwa ya ngono, afya ya uzazi, madawa ya kulevya na unyanyasaji wa kijinsia.

Alianza kwa kusema: “Ni kweli mimi ndiye niliyetendewa ukatili ule. Natamani kujiua kwani mambo yale nayasikia tu usiombe yakukute.
“Nimefedheheka sana, sina mahala pa kuficha aibu hii kubwa. Kila nikikumbuka kuwa nina wake wawili na watoto, wazazi, marafiki na ndugu, bora hata wangeniua kuliko kuniacha nazidi kudhalilika hivi.
“Siku ya tukio ilikuwa Jumamosi ya Agosti 23, mwaka huu. Kuna mwanamke mmoja anaitwa mama Lilly alinipigia simu. Kwanza alikuwa akinipigia simu mara kwa mara wiki moja kabla ya tukio akinieleza kwamba ana shida na mimi, alisema mume wake amekuwa akimnyanyasa kijinsia.

“Siku hiyo, saa tatu asubuhi mama Lilly alinipigia simu huku analia, akasema  kwamba mumewe kampiga na kumfukuza nyumbani hivyo anaomba kuonana na mimi kwa ajili ya ushauri ila alitaka tukutane naye maeneo ya Mtongani, Mbagala au Tandika.
“Nilikataa, nikamwambia aje kwenye Ukumbi wa Maembe ninakotoaga mafunzo mbalimbali kwa vijana. Ukumbi huo upo karibu na nyumba hiyo ya kulala wageni kulikotokea tukio.
“Huyu mwanamke namfahamu kwani kipindi cha nyuma alikuwa na stationary karibu na maeneo haya, nilikuwa nikimtengenezea kompyuta lakini miaka miwili iliyopita alihama na sikujua alipo hadi hivi karibuni aliponipigia simu.

“Basi, nilipomwambia aje yeye maeneo haya, aliamua kunifuata. Alifika saa saba mchana huku akibubujikwa machozi, nilimsikiliza kwa makini matatizo yake mwishowe aliniomba nimkopeshe shilingi laki moja ili aende kwao, nilimjibu kwa pale sikuwa nazo labda mpaka Jumatatu.
“Akasema kama ni hivyo basi nimsaidie sehemu ya kulala ili kesho yake aondoke kwenda kwa dada yake. Nilimuonea huruma, nilimchukulia chumba, nikamwambia kama kutakuwa na tatizo anipigie simu. Wakati najiandaa kutoka chumbani aliendelea kuongea maneno mengi sana ya kunifanya niendelee kuwepo.
“Wakati huo alikuwa akituma ujumbe wa simu sehemu nisiyoijua. Sasa nilipoagana naye, ile natoka tu, mlangoni niliona wanaume sita wakanirudisha chumbani na kufunga mlango.“Wakaniambia niwape namba yangu ya akaunti ya benki na password ya simu yangu kwani walijua kwamba tayari nimetumiwa fedha kutoka nje ya nchi kutoka kwa wafadhili.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP, Mary Nzuki akiwa kazini.
“Niliwaambia sina akaunti, wakanipiga sana, ikabidi niwaongopee kwamba nyumbani nina shilingi laki tano, wakaniambia niwaelekeze nyumbani, nikafanya hivyo. Wawili kati yao waliondoka na pikipiki hadi kwangu kuchukua fedha, wengine wakawa wamenizuia chumbani na kunitishia nikipiga kelele ndiyo mwisho wa maisha yangu.
“Wale walipofika kwangu walimwambia mke wangu awape laki tano na walimtaka aongee na mimi kwa simu huku nikiwa chini ya ulinzi. Mke wangu aliwaambia hana fedha hizo ana laki moja tu, nilimwambia awape.“Waliporudi  na shilingi laki moja walisema nimewadanganya, wakaniadhibu na kunivua  nguo, wakanilawiti kwa zamu na kunilazimisha kuwafanyia mambo ambayo ni tabu hata kuyasema huku wakinipiga picha.
“Baada ya kumaliza walichukuwa laptop, nguo na simu wakaondoka huku wakiniambia ifikika Jumatatu, yaani siku moja baada ya tukio niwape shilingi milioni moja la sivyo wanaweka picha zangu mtandaoni.
“Hata hivyo, baada ya kukosa hizo fedha waliziweka picha mtandaoni, ikawa napigiwa simu na watu mbalimbali walioziona.“Waliponiacha pale chumbani nikiwa  sina nguvu, nilichukuwa shuka nilijikokota mpaka kwa meneja wa gesti na kumweleza. Alinipa nguo yake ili niweze kwenda Kituo Kidogo cha Polisi cha Minazi Mirefu kutoa taarifa na baadaye  Buguruni na kufungua kesi yenye jalada namba BUG/RB/8520/2014 Kujipatia Fedha kwa Njia ya Udanganyifu lakini baadaye ikaongezwa shitaka lingine la kulawiti.
“Kinachonishangaza ni kwamba iweje wanaume hao sita waingie na kutoka bila wenye gesti kuwabaini?” alihoji mwanaume huyo.
Naye mmiliki wa nyumba hiyo ya wageni alikiri kupokea taarifa ya kutokea kwa tukio hilo na kudai kwamba ni la aibu na kusema suala hilo linashughulikiwa na jeshi la polisi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP, Mary Nzuki alipohojiwa na mmoja wa waandishi wa habari hii ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari watuhumiwa wanne wanashikiliwa Kamanda Nzuki aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Erick Kasila, Sanifa Sadik, Shela Sadik na Juma Richard.
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate