EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, October 16, 2014

CRISS MAUKI, JOKATE MWEGELO, SIZA MA-MC SIKU YA MSANII

Jokate Mwegelo
Dk. Criss Mauki
BALOZI wa Redd’s Jokate Mwegelo, Dk. Criss Mauki wametangazwa kuwa washehereheshaji katika maadhimisho ya Siku Ya Msanii Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Siku Ya Msanii, Justin Jones alisema kutakuwa na washehereheshaji watatu katika siku hiyo ambapo Criss, Jokate wataungana na MC mwingine Siza Daniel katika kupendezesha shughuli hiyo. 

“Tulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao walitajwa ili wawe Ma-MC katika shughuli yetu lakini baada ya kutafakari tukabaki na majina haya matatu ambao wanaingia kwenye historia ya kuwa washehereshaji wa kwanza katika Siku hii ya kwao,” alisema. 
Akizungumzia taarifa ya kuchaguliwa kwake kuwa MC wa Siku Ya Msanii, Dk. Mauki alisema alifurahishwa na uamuzi huo kwa kuwa ni tukio kubwa ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza nchini. 
“Nilifurahi sana, kwangu si mara ya kwanza kufanya kazi na Haak Neel Production, lakini kwa hili Tamasha ni la kitaifa na linafanyika kwa mara ya kwanza, kwangu ni furaha kuhusishwa nalo, ni heshima kwangu, ingawa nimeshafanya shughuli kwenye majukwaa mengine lakini hili litaniongezea heshima, zaidi,” alisema. 
Dk. Mauki ni mwanasaikolojia ambaye amekuwa akitoa mafunzo mbalimbali kupitia vipindi mbalimbali vya radio, televisheni mijadala na kwenye magazeti.Jokate amekuwa akifanya shughuli za ushehereshaji katika shughuli mbalimbali ambapo pia ni mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha TV1 cha mjini Dar es Salaam  akiwa na pia anafanya kazi na DSTV ya Afrika Kusini. 
Ni mrembo ambaye aliweza kufanya vizuri alipokuwa Balozi wa kinywaji cha Redds mwaka 2006, ambapo ilidhaniwa kuwa ndiye angekuwa Miss Tanzania lakini alikuwa Miss Photogenic katika mashindano ya Miss Tanzania mwaka huo.  Kwa upande wake Siza, alikuwa mtangazaji wa kituo cha Clouds FM, na baadae kuwa MC katika shindano la Bongo Star Search pamoja Dume Challenge. 
Siku Ya Msanii Tanzania inaandaliwa na Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo imedhaminiwa na New Habari (2006) LTD kupitia magazeti ya Dimba, Bingwa, Mtanzania na The African, Channel Ten, Magic FM, Michuzi Media, PSPF, Proin Tanzania, Azam Media na CXC.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate