EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, November 11, 2014

ASKOFU ANASWA NA UNGA!

Stori: MAKONGORO OGING’ na Haruni Sanchawa                KIMENUKA! Vigogo wa madawa ya kulevya wakiwemo viongozi wa dini sasa wanaanza kupukutika kutoka kwenye mstari wa siri huku baadhi yao wakikimbilia nje ya nchi kufuatia oparesheni kali inayofanywa na Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulenya Tanzania kuwanasa kila kukicha, Uwazi  lina mchoro kamili.Askofu Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Hivi karibuni kikosi hicho kimemkamata askofu (mwangalizi mkuu wa kanisa) aliyetambulika kwa jina la Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria ambaye ana kanisa la kiroho maeneo ya Sinza jijini Dar.
Jina la kanisa hilo limedhibitiwa na vyombo husika kwa sababu ya uchunguzi zaidi na uhalali wake wa kuwepo nchini.
SIKU YA TUKIO
Vyanzo vyetu makini ndani ya kikosi kazi vinaeleza kwamba, mchungaji huyo alikamatwa Oktoba 31, mwaka huu saa kumi usiku Tegeta wilayani Kinondoni, Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya ‘unga’ aina ya heroine kilo 35.
KAMA UNGEINGIA SOKONI
 Habari za ndani kutoka kwenye oparesheni hiyo zinasema kuwa, endapo unga huo ungeingia sokoni na kununuliwa, basi mtumishi huyo wa Mungu angevuna kitita cha zaidi ya shilingi bilioni mbili.
NYUMBA ALIYONASIWA YA PROFESA
Mchungaji huyo ambaye serikali imeanza kazi ya kulichunguza kanisa lake, alidakwa na mzigo huo haramu kwenye makazi aliyopanga ambayo ni nyumba ya profesa mmoja wa chuo kikuu, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Askofu akiwa chini ya ulinzi.

WASHIRIKA NAO WADAKWA
Kwa mujibu wa chanzo, kamatakamata ya mchungaji huyo pia iliwakumba watuhumiwa wengine ambao ni Walyat Khan raia wa Pakistani, Chuksi Sylvester Agbazuo na Tony Olafor wote raia wa Nigeria na inadaiwa kwamba walikuwa wakikamatwa maeneo mbalimbali na kutoroka.
HABARI NYETI
Habari za siri ambazo Uwazi ilizinasa zinadai kuwa,  watumishi wa Mungu waliokuwa kwenye orodha ya kunaswa walikuwa wengi lakini  wamekimbilia nje ya nchi na kikosi hicho kimeshawasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kwa ajili ya kuwasaka na kuwatia nguvuni.
MAJINA MAPYA MEZAN KWA NZOWA
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa amekabidhiwa majina ya vigogo wakiwemo viongozi wa dini ambao ni sugu katika biashara hiyo. Mbali na majina hayo,  pia amepewa ratiba zao za safari za kibiashara hivyo kilichobaki ni kuwafuatilia na kuwakamata na ushahidi ili kuhakikisha kwamba hawawezi kupona mahakamani.
MTANDAO HATARI
Habari zaidi zinadai kuwa, siku za hivi karibuni, Kamanda  Nzowa amekuwa akifumua mtandao wa watu wazito katika biashara hiyo na imebainika kuwa vigogo hao wana mtandao mkubwa serikalini ikiwemo wizara ya mambo ya ndani ambao wanawalinda kwa kupewa mamilioni ya pesa kwa ajili ya usimamizi wa upitishwaji wa biashara hiyo haramu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar.
“Unajua zamani viongozi hao serikalini walikuwa wakimsumbua Kamanda Nzowa ili awaachie watuhumiwa waliokamatwa na unga bila mafanikio, lakini sasa wameshamsoma kiasi kwamba hata wakikamatwa hawampigii simu tena,” kilisema chanzo kingine.
Dawa za kulevya alizokutwa nazo askofu huyo.
WATOTO WA VIGOGO
Habari nyingine zinadai kuwa, Kamanda Nzowa pia ana majina ya watoto wa vigogo wa serikali wanaojihusisha na biashara hiyo na anayafanyia kazi.
KUMBUKUMBU
Kukamatwa kwa askofu huyo kumekuja baada ya kukamatwa kwa vigogo ambao ni viongozi wa dini katika makanisa ya kilokole.
Januari 11, mwaka huu, Askofu Moris Charles alidaiwa kukamatwa na polisi maeneo ya Chinga Mbili mkoani Lindi akiwa na kilo 210 za madawa ya kulevya aina ya heroine yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4, kesi yake bado inaendelea mahakamani mkoani humo.
Juni 8, 2011 polisi walifanikiwa kumkamata Mchungaji Kapupu Denis Okechuku wa kanisa la kilokole lililopo Kinondoni Biafra akiwa na kilo 81 za cocaine, kesi yao bado ipo Mahakama ya Kisutu, Dar.
Nyumba aliyokutwa askofu huyo.
KAMANDA NZOWA
Uwazi lilipomtafuta Kamanda Nzowa ofisini kwake juzi, alisema kuna watu wanne waliokamatwa Tegeta wakiwa na kilo 35 za madawa ya kulevya aina ya heroin na kuna wengine wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo.
“Kwa sasa nisingependa kuzungumzia sakata hilo kutokana na sababu za kiupelelezi kwani kuna wengine tunawatafuta na nitahakikisha wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria, nawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao,” alisema Nzowa.
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate