Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dlamini Zuma
Viongozi wa juu wa maswala ya biashara barani Afrika wameanzisha mfuko wa kusaidia nchi zilizoathiriwa na ugonjwa wa Ebola.
Kiasi cha
dola milioni 28.5 zilipatikana katika mkutano wa harambee mjini Addis
Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuwapeleka wahudumu wa afya nchini
Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Wataalam wanasema kama wanataka kukabili ugonjwa huu kwa kasi hakuna budi kuanza na nchi hizo tatu.
Takriban watu 5000 kati ya 14,000 wamepoteza maisha kutokana na Virusi vya ugonjwa huu hasa nchini Liberia.
Akiongea
baada ya mkutano wa Addis Ababa, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Dlamini
Zuma amesema rasilimali zilizokusanywa zitakua sehemu ya mchakato wa
kupambana na ugonjwa huo siku za usoni.
mkutano
wa Addis Ababa umefanyika wakati Liberia ilipotangazwa na Shirika la
madaktari wasio na mipaka,MSF kuwa imefanikiwa kupunguza idadi ya
maambukizo mapya.
Hata hivyo shirika hilo limesema bado Ebola iko kwa kiasi kikubwa nchini Guinea na Sierra Leone.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment