EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, November 3, 2014

HOSPITALI YA KAIRUKI YAPATA TUZO YA UBORESHAJI VIWANGO VYA HUDUMA YA AFYA


 Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu akiwa amebeba tuzo aliyokabidhiwa na na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati). Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid.
Picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ameukabidhi uongozi wa Hospitali ya Kairuki (KH) tuzo ya waliofanya vizuri katika vigezo mbalimbali vya uboreshaji viwango vya huduma ya Afya katika mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya uliofanyika wiki iliyopita (Octoba 31-2014) katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu alisema sifa ya mafanikio yao mpaka wakapata tuzo hiyo yanatokana na mafunzo  kwa wafanyakazi wa Hospital wapatao 20 yaliyoendeshwa na Wizara ya afya ikishirikiana na Jhpiego,CDC na PEPFAR.

Dk. Mchomvu aliongeza kuwa mafunzo kuendelea kutolewa na wakufunzi wa ndani (inhouse training), kuundwa kwa timu maalum ya ndani kwa ajili kufanya ukaguzi wa kushtukiza ndani na utayari wa KH kushirikia katika zoezi la udhibiti na uzuiaji wa maambukizi.

Aidha, Dk. Mchomvu alieleza kuwa siri nyingine ni ushirikiano mzuri baina ya manegimenti ya KH na timu ya wakaguzi toka wizara ya Afya katika kutekeleza maagizo na mapendekezo na kuyafanyia kazi.

“Kwa upande wetu maeneo yaliyofanya vizuri katika zoezi ili ni pamoja na mashine bora za kuuwa vijidudu (sterilization unit) na eneo zima katika kitengo hicho, eneo la kuifadhi/ kutenganisha na usafirishaji wa taka hatarishi, taka mbichi na taka mchanganyiko pia chumba cha upasuaji kufuata taratibu stahiki za kimataifa katika kuzithibiti maambukizi,” alisema Dk. Mchomvu.

Aliongeza kuwa wakati huohuo KH imezindua kampeni maalum za muda mrefu katika kuchunguza na kutibu magonjwa yasiyoambukiza, mfano saratani ya matiti, saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya tezi dume (prostate). Saratani hizi ndizo zinazoongoza kwa  hapa nchini.
Moja ya mashine za kisasa za kupima saratani ya matiti katika Hospitali ya Kairuki.

“Lakini pia KH imezidi kuboresha huduma katika vitengo vya macho, sikio, pua na  koo kwa kupata mitambo ya kisasa katika nyanja hizo,” alisema Dk. Mchomvu.Aliongeza kwa kusema kuwa KH imezindua wodi mpya ya kisasa hasa kwa ajili ya wanachama  wa mfuko wa Bima ya taifa ya afya. (NHIF) na wodi maalum ya watoto.

Wengine waliotunukiwa tuzo hizo za uboreshaji wa huduma za afya ni Hospitali ya Bugando-Mwanza pamoja na Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). 

Tuzo hizo zilitolewa na Wizara ya Afya wakishirikiana na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Marekani (CDC) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate