Stori: Musa Mateja KESI
ya kuua bila kukusudia inayomkabili mtoto mzuri wa Bongo Movies,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ imewekwa kiporo kufuatia kuwepo kwa kesi nyingi
za mauaji mahakamani, Risasi Mchanganyiko limetonywa.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa wa kesi hiyo
kusikilizwa tena Februari mwakani kutokana na mlolongo mkubwa wa kesi za
mauaji zilizopo Mahakama Kuu ya Tanzania.
Chanzo hicho ambacho kipo ndani ya kamati ya majaji wanaoshughulikia
kesi hiyo, kimenyetisha kuwa kesi ya Lulu itakuwa ngumu kusikilizwa
wakati huu kwani mbali na wingi wa kesi mahakamani hapo, lakini pia
majaji na mawakili watakwenda likizo.
“Ujue kesi ya Lulu ilikuwa miongoni mwa ambazo zingesomwa kabla ya
mwaka huu kuisha, ila kulingana na vikao vya majaji inaonyesha wazi
kabisa mwaka huu itakuwa ngumu hata Januari haitawezekana kwani wana
kesi kama tatu za mauaji na baada ya hapo watakwenda likizo sambamba na
mawakili kwani nao ndiyo kipindi chao cha likizo,” kilisema chanzo
chetu.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi
wake, Steven Kanumba, Aprili 7, 2012 maeneo ya Vatican-Sinza jijini
Dar.Kifo cha Kanumba kilichotokea nyumbani kwake, kilidaiwa kilitokana
na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa
ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
No comments:
Post a Comment