Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
NABII wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera amesema uchaguzi mkuu ujao utakuwa balaa kubwa kufuatia maono anayoyaona wakati akishiriki ibada katika nyakati mbalimbali, Risasi Jumatano linakupa mkanda kamili.
NABII wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera amesema uchaguzi mkuu ujao utakuwa balaa kubwa kufuatia maono anayoyaona wakati akishiriki ibada katika nyakati mbalimbali, Risasi Jumatano linakupa mkanda kamili.
Akizungumza wakati wa ibada kanisani kwake na baadaye na waandishi
wetu Novemba 16 mwaka huu, Nabii Yaspi alisema kuna mgongano mkubwa
miongoni mwa watu wanaotajwa kugombea urais, ili kumrithi rais Jakaya
Kikwete ambaye alimwelezea kama kiongozi anayemuona kiroho kila mara.
“Nilimuona katika maono yangu kama mtu aliye kwenye majaribu makubwa
kiroho, nikaandaa maombi hapa kanisani na tukamuombea kwa muda wa nusu
saa na tunashukuru Mungu hali yake inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa
upasuaji wa tezi dume nchini Marekani. Bado namuona akiwa na maumivu
kuanzia sehemu za kiuno, uti wa mgongo na shingoni mwake.
“Hivi sasa ninapomuombea atasikia moto unawaka na kupita kwenye
sehemu hizo na kuwa mzima kabisa. Tunamuombea baraka na uzima rais ili
aweze kukabidhi madaraka vizuri kwa rais ajae,”alisema Nabii huyo na
kuongeza kuwa alilazimika kumuombea rais ili asipatwe na madhara kwani
kama hali hiyo ingetokea, kungekuwa na vurugu kubwa kuelekea wakati wa
Uchaguzi mkuu.
Waandishi wetu waliokuwa eneo la tukio walimshuhudia Nabii Yaspi
akiwa ameshika picha ya Rais na waumini wake wakizama katika maombi kwa
ajili ya Rais Kikwete huku na walipomaliza alisema tatizo lake
limemalizika.
Kana kwamba haitoshi, Nabii huyo alisema baadhi ya wagombea urais
wanapita kwa waganga wa kienyeji lakini akasema hawatafanikiwa kwa kuwa
yeye anaomba Rais ajaye atoke kwa Mungu kwa kuwa yeye atakuwa nyuma ya
mgombea huyo bila kujali chama anachotoka.
Nje ya ukumbi wa kanisa, Nabii huyo alizungumza na waandishi wetu
ambao walimuuliza kuhusu jinsi anavyoona kuelekea uchaguzi mkuu wa
mwakani.Vipi kuhusu utafiti wa Twaweza
Kuhusu utafiti uliotolewa hivi karibuni kuhusiana na uchaguzi mkuu
kama ulivyowasilishwa na taasisi ya Twaweza, ambao umewagawa wananchi,
Nabii huyo alisema anaunga mkono kwani umefanywa kwa usahihi kwa vile
ndivyo hata yeye anavyoona.
“Utafiti umefanywa vizuri na nadhani kila kitu kipo kama
kilivyoainishwa, lakini kama walivyosema wenyewe kwenye ripoti yao,
upepo unaweza kubadilika wakati wowote maana miujiza ya Mungu huja bila
kutarajiwa,” alisema.Nani atashinda Urais?
“Hivi unauliza swali kama hilo kweli wakati huu? Ripoti iliyotolewa
imemaliza kila kitu na majibu yako wazi kabisa,” alisema nabii huyo bila
kutoa ufafanuzi zaidi.
Utafiti uliotolewa na taasisi hiyo ya Twaweza uliotolewa hivi
karibuni, ulisema kuwa endapo Uchaguzi mkuu wan chi ungefanyika hivi
sasa, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa angeibuka mshindi, huku
akifuatiwa kwa karibu na Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda na Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akiibuka katika nafasi ya tatu.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment