SIKU chache baada ya Jeshi
la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania
kumkamata mfanyabiashara bilionea Mharami Mohamed Abdallah ‘Chonji’
mkazi wa Magomeni, Mtaa wa Kondoa jijini Dar akidaiwa kukutwa na unga,
jeshi hilo linamhenyesha anayedaiwa kigogo mwingine wa unga ambaye ni
mwanamke.
Kamanda wa kitengo hicho, SACP Godfrey Nzowa, wiki iliyopita aliimbia
Uwazi kwamba mwanamke huyo, Christina Naphtali Kigaye (pichani), mkazi
wa Mikocheni, Dar alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi lake.
Kamanda Nzowa alisema, Christina amekuwa akitajwa na watu wengi
wanaokamatwa na unga kuwa, yeye ndiye kigogo wa unga na amekuwa
akiwabebesha mzigo na kuwatuma sokoni nje ya nchi.
Kamanda Nzowa alisema siku ya tukio kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, saa tatu asubuhi ya
Oktoba 29, mwaka huu, mtuhumiwa huyo akitokea nje ya nchi alinaswa baada
kitengo chake kutonywa na watuhumiwa wengine ambao tayari
wameshakamatwa lakini wakawa wanaijua ratiba yake.
“Pamoja na kwamba anadai kuwa anafanya biashara ya kuuza nguo na simu
lakini hizo amejiegesha tu. Kwa mujibu wa watuhumiwa waliokamatwa na
unga wamemtaja kwa asilimia kubwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.
“Kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi yake na utakapokamilika hatua
zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwa na pamoja na kumpandisha
mahakamani,” alisema Kamanda Nzowa.
Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mwanamke
huyo alipelekwa makao makuu ya kitengo cha kuzuia madawa hayo Kilwa Road
na kuhojiwa maswali mengi ambayo yalimtoa jasho.
“Alihojiwa kwa saa nyingi hadi akatokwa na jasho, maswali yalikuwa mazito,” alisema mtoa taarifa wetu.
“Alihojiwa kwa saa nyingi hadi akatokwa na jasho, maswali yalikuwa mazito,” alisema mtoa taarifa wetu.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment