CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Kijana Mohamed Said almaarufu Ngwea feki, anayefananishwa na aliyekuwa staa wa Bongo Fleva, marehemu Alberth Mangweha ‘Ngwea’, ameingia katika mzozo mkali na ndugu zake akidaiwa kugombea maiti ya mama yake mzazi, Mariamu Enock (54).
Kijana Mohamed Said almaarufu Ngwea feki, anayefananishwa na aliyekuwa staa wa Bongo Fleva, marehemu Alberth Mangweha ‘Ngwea’, ameingia katika mzozo mkali na ndugu zake akidaiwa kugombea maiti ya mama yake mzazi, Mariamu Enock (54).
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo
lilijiri kwenye makazi ya familia hiyo, Tandale, Dar hivi karibuni
ambapo mama huyo alifariki dunia kwa kuugua kwa muda mrefu.
Ilidaiwa kwamba, baada ya kifo hicho,
uliibuka mzozo ambapo ndugu wa upande wa mama yake walitaka mwili
wakaupumzishe mkoani Iringa huku Ngwea feki akitaka uzikwe Dar.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alitaka iwe hivyo kwa sababu alikuwa na
mama yake muda wote na alitumia gharama kubwa kumtibu.
Akizungumza na mwanahabari wetu kuhusiana
na sakata hilo, msemaji wa familia hiyo, Laurence Enock ambaye ni kaka
wa marehemu (yaani mjomba wa Ngwea feki), alisema: “Sisi kama familia
tumeamua kumsafirisha ndugu yetu kwenda kumzika Iringa, ndiko kuna
mashamba ya familia yetu lakini Mohamed (Ngwea feki) amekataa.”
Alisema kwamba, baada ya vuta nikuvute
ndipo Ngwea feki akadai alipwe shilingi laki tatu (300,000/=) alizotumia
kumtibu mama yake wakati anaumwa.Kwa upande wake, ndugu wa Ngwea feki
aliyefahamika kwa jina la Hassan Said alionekana kutomuunga mkono ndugu
yake.
Hassan alisema: “Mimi siko tayari kugawana vitu vya mama yangu kwa
kuwa ndugu yangu amekataa mwili wa mama usisafirishwe hadi alipwe fidia
yake hivyo imebidi tuuze vitu vya mama ili alipwe hiyo laki tatu.
Wa pili kushoto ni msemaji wa familia hiyo, Laurence Enock ambaye ni kaka wa marehemu (yaani mjomba wa Ngwea feki)
Alipofuatwa Ngwea feki ili kusikia upande wake aligoma kutoa ushirikiano: “Siko vizuri kwa sasa nicheki baadaye.”
Kwa mujibu wa baba wa marehemu, Enock
Mayenje, mjukuu wake huyo amekuwa akijitenga na familia hivyo hawezi
kumlazimisha ila amesikitika kwa kitendo chake cha ‘kuwauzia’ maiti ya
mama yake mzazi.
Kamanda wa Ulinzi Mtaa wa Mkunduge, Tandale jijini Dar, Yusuph Banda,
amekiri kutokea kwa tukio hilo na wamekubaliana kuuzwa kwa vitu vya
marehemu ili gharama hizo zilipwe kwa Ngwea feki ili mwili huo
usafirishwe kwenda Iringa kwa mazishi.Kujua mengi zaidi kuhusu tukio
hilo, tembelea www.globaltv.tz
No comments:
Post a Comment