MAKATIBU WAKUU WA WIZARA
Rais
Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua
Makatibu Wakuu wanne wapya na kuhamisha mmoja, uteuzi uliomuondoa Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo.
Pallangyo
sasa anakua Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, nafasi ambayo inatafsriwa
kuwa adhabu, siku chache baada ya vyombo vya habari ikiwamo FikraPevu
kuibua kashfa ya uhaba wa dawa katika hospitali kubwa za serikali.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.
Taarifa
iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa walioteuliwa ni
pamoja na Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii kuchukua nafasi ya Pallangyo.
Katika
uteuzi huo Dkt. Yohana Budeba anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo
ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Utalii na Maliasili.
Kabla
ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt.
Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na
Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na
Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji
kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Aidha,
taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi Maimuna Tarishi
kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Katiba na Sheria
Adoh
Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba amepanda na
kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa
Mkoa wa Geita anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt.
Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro anahamishiwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Wakati
huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA kuchukua nafasi ya Dkt.
Meru.
Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment